Ujumbe wa Tanzania katika majadiliano, kutoka kushoto ni Mhasibu Mkuu wa Serikali Bi. Mwanaidi Mtanda, Kamishna Idara ya Sera Bw. Beda Shallanda, Mkurugenzi wa Utafiti na Sera za Uchumi wa BOT Dkt. Joseph Masawe na Bw. Said Magonya Kamishna wa Fedha za Nje akielezea jambo.
Waziri wa Fedha wa Zanzibar Mhe. Yusuph Mzee kulia, akisoma kwa makini taarifa zitakazowasiliswa katika mikutano hiyo wengine ni wajumbe kutoka Tanzania.
Kutoka kushoto ni Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Wiliam Mgimwa, Balozi wa Tanzania Marekani na Mexico Mhe. Liberata Mulamula, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Silvacius Likwelile, Mkurugenzi wa Idara ya kupunguza Umasikini MKUKUTA Bi. Anna Mwasha pamoja na Kamishna Mkuu wa TRA Bw. Harry Kitilya wakisikiliza kwa makini.
Ujumbe wa Tanzania wakisikiliza kwa makini hoja zinazotolewa na Waziri wa Fedha hayupo pichani ambaye ni mwenyekiti wa kikao hicho.
Kutoka kulia ni Katibu Mtendaji Ofisi ya Rais Tume ya Mipango Dr. Philip Mpango, Naibu Gavana wa BOT Bi. Natu Mwamba na Mchumi wa Benki Kuu Bi. Sauda Msemo wakisikiliza kwa makini.
Kutoka kushoto ni Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Wiliam Mgimwa, Balozi wa Tanzania Marekani na Mexico Mhe. Liberata Mulamula pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Silvacius Likwelile akitoa ufafanuzi.
Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Wiliam Mgimwa akiwa katika majadiliano na ujumbe wa Tanzania kuhusu maandalizi ya mikutano na Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa.
Kutoka kushoto ni Kamishna wa Idara ya Sera Bw. Beda Shallanda akiteta jambo na Mkurugenzi wa Utafiti na Sera za Uchumi wa BOT Dkt. Joseph Masawe.
Balozi wa Tanzania Marekani na Mexico Mhe. Liberata Mulamula akimsikiliza kwa makini Afisa Mwambata anayeratibu masuala ya Uchumi, Biashara, na Uwezeshaji ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa Bw. Paul Mwafongo.
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA FEDHA
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
MIKUTANO
YA MWAKA YA SHIRIKA LA FEDHA LA KIMATAIFA NA KUNDI LA
BENKI
YA DUNIA YAANZA.
Bodi ya Magavana wa kundi la Benki ya Dunia ( Benki ) na Bodi ya Magavana wa Shirika la Fedha la Kimataifa ( Mfuko) kwa kawaida hukutana mara moja kwa mwaka kujadili kazi za Taasisi zinazowahusu. Mikutano hii hufanyika mjini Washington DC kwa miaka miwili mfululizo na kwa mwaka wa tatu hufanyika kwa nchi mwanachama.
Waziri wa Fedha wa Tanzania Mhe. Dkt. Willium Mgimwa , Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Dr. Silvanus Lekwilile pamoja na Gavana wa Benki Kuu Prof. Benno Ndulu wao ni Magavana wa mikutano hiyo. Nchi karibu zote zimeshawasili katika mikutano hii.
‘Lengo la mikutano hii kwa nchi ya Tanzania, inatupa nafasi ya kuweza kujadiliana na Benki ya Dunia pamoja na Shirika la Fedha la Kimataifa kuhusiana na hali ya uchumi kwa maana ya sera za fedha na sera za mapato na matumizi. Nia yao kubwa ni kutusaidia na kusikia tuna mawazo gani na maeneo gani wanaweza wakatusaidia katika kuboresha na kuangalia kwamba nchi yetu inaendelea kufanya vizuri’. Haya yamesemwa na Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Wiliam Mgimwa alipokuwa akijadiliana na ujumbe kutoka Tanzania.
Aidha Mhe. Dkt. Mgimwa alisema kuwa, Katika mazungumzo na Benki ya Dunia pamoja na Shirika la Fedha la Kimataifa, ujumbe wa Tanzania utawasilisha hali halisi ya utendaji wa kiuchumi wa Tanzania na hali ya matumizi na mapato ya fedha na mambo yanayohusiana na taasisi zinazoendesha nishati kama vile Shirika la umeme Tanazania (Tanesco) na shirika la maendeleo ya mafuta Tanzania (TPDC) pamoja na kutazama mienendo ya madeni yetu na mwenendo wa mapato kwa ujumla.
Hali ya hewa mjini hapa ni ya manyunyu na mvua za hapa na pale.
Imetolewa
na:
Ingiahedi
Mduma
Msemaji
Mkuu
Wizara
ya Fedha
Washington
D.C
7/10/2013
No comments:
Post a Comment