ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, October 23, 2013

MOTO ULIVYOSIMAMISHA MSAFARA WA WAHESHIMIWA ENEO LA MUFINDI

Moto mkubwa ukiteketeza msitu wa Sao Hill Mufindi: 
hapa askari wakishuka kuingia katika moshi mzito kuangalia usalama wa rais katika eneo hilo ambalo moshi mzito ulitanda barabarani
Msafara ukipita eneo hilo salama huku kulia ni askari wa JKT mafinga wakizima moto huo 
YAKIWA ni masaa takribani mawili kupita kutoka Rais Jakaya Kikwete kufanya kikao chake cha majumuisho ya ziara yake na viongozi wa mkoa wa Njombe na kuwataka kuchukua hatua katika kuthibiti moto ili kuepusha ukame ,moto mkubwa umezuka katika msitu wa Taifa wa Sao Hill Mufindi na kupelekea msafara wa Rais kusimama kwa muda kiusalama kutoka na moshi mzito uliotanda barabara kuu ya Iringa Mbeya .
Moto ulio ulioanza kuwaka mida ya saa nane mchana ulizuia kwa muda kama dakika tatu hivi msafara wa Rais Kikwete kufimama katika eneo la Changalawe mjini Mafinga umbali wa mita 2 kufika njiapanda ya kuingia ofisi ya mkuu wa wilaya ya Mufindi na Ikulu ndogo ya wilaya ya Mufindi.
Kutokana na tukio hilo la moto msafara wa rais Kikwete ulisimama na baada ya maofisa usalama kushuka na kutazama usalama zaidi wa msafara huo ndipo walioruhusu msafara huo kuendelea .
Hata hivyo jitihada kubwa zilionekana kufanywa na kikosi cha askari wa JKT Mafinga pamoja na wananchi ambao walikuwa wakizima moto huo .
Huku vyombo vya usafiri yakiwemo mabasi ya abiri yanayosafiri kutoka Dar es Salaam kuwenda mikoa ya kusini na nchi za kusini mwa Tanzania yakikwama kuendelea na safari kutoka na moto huo kushikakasi na moshi mzito kutanda barabara 
Mkuu wa mkoa wa Iringa Dr Christine Ishengoma alisema kuwa uongozi wa mkoa tayari umeagiza mkuu wa wilaya ya Mufindi kuwasaka waliohusika na uchomaji moto huo ili kuchukulia hatua kali.
Mkuu huyo wa mkoa alisema kuwa mkoa wa Iringa umekuwa ukichukua hatua kali kwa wale wote wanaoanzisha moto kichaa kama huo hivyo kupitia ofisi ya mkuu wa wilaya ya Mufindi wahusika watasakwa popote walipo .
Mbali na hilo mkuu huyo amelipongeza jeshi la JTK Mafinga kwa kuchukua hatua za haraka katika kukabiliana na moto huo huku akisema madhara zaidi yatokanayo na moto huo yatatolewa baada ya moto huo kuthibitiwa . Picha zote na Mzee wa Matukio Daima

No comments: