Ni siku zisizozidi 5 toka bodi ya Utalii Tanzania kutangaza kwamba Tanzania kwa mwaka 2012 peke yake Utalii umeingiza shilingi Trilioni 2.69 kwenye pato la taifa ikiwa ni ongezeko la asilimi 24 ikilinganishwa na mwaka 2011 na kwamba Watalii wanaotembelea Tanzania kutoka nje ya nchi wamekua wakiongezeka kila mwaka kutoka Watalii laki nane na elfu 67,994 mwaka 2011 mpaka milioni moja na elfu sabini na saba 58 mwaka 2012.
Tanzania ina mbuga nzuri sana za Wanyama na sehemu nyingine nzuri za kutengeneza pesa zinazotokana na Utalii na ninaamini kama zikitangazwa kwa nguvu na kufika kunakotakiwa hata hiyo Trilioni 2.6 kwa mwaka itakua ndogo, yani mkwanja utaingia mrefu zaidi.
Nimefurahi kwenda Cinema na kutazama movie mpya ya Baggage claim na kukutana na sehemu ya movie hiyo ambayo jamaa alikua anaongea na mrembo akitaka azunguke nae sehemu mbalimbali duniani ikiwemo kuitembelea mbuga ya wanyama ya Serengeti.
Nilijua hii ishu ingekua kubwa kwangu tu ila kiukweli watu niliokua natazama nao movie nao walifurahi tena wengine wengi tu kupiga makofi ya midadi nikiwemo mimi… ni movie ambayo ndani yake kuna mastaa kama Trey Songz, Paula Patton na Lauren London.
Mwanaume huyu Djimon Honsou ndio alisikika akimwambia Paula Patton kuhusu kwenda Serengeti japo safari yenyewe haikufanikiwa, Djimon ni mzaliwa wa Benin miaka 49 iliyopita.
Hii sio mara ya kwanza kwa Tanzania kuingia kwenye headlines kwa kutajwa na mastaa wa majuu, nakumbuka kwa harakaharaka miongoni mwa waliowahi kuitaja ni pamoja na mwigizaji wa movie za Action Steven Seagal alieitaja Dar es salaam na mtangazaji Oprah ambae alikuja Tanzania siku kadhaa zilizopita.
No comments:
Post a Comment