Mamia ya wakazi wa wilaya ya Hai kwenye mkoa wa Kilimanjaro na Karatu Arusha wamejitokeza kwa wingi kumzika Mama mzazi wa Mwandishi wa habari wa ITV Ufoo Saro, Anastazia Saro katika viwanja vya kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzania usharika wa Uraa.
Kiongozi wa msafara Alelio Swai amesema baada ya uchunguzi kufanywa kwenye mwili wa mama huyu, imefahamika ni risasi tano alipigwa na ndio maana haikua rahisi kuhimili na kupona kwenye shambulio hilo ambalo alipigwa risasi za tumbo pamoja na kifuani.
Madaktari baada ya uchunguzi ndio waliruhusu Marehemu kuzikwa October 16 2013 baada ya kufariki October 13 saa kumi na mbili asubuhi akiwa na umri wa miaka 56 ambapo ameacha mtoto mmoja ambae ni Ufoo Saro pamoja na mjukuu mmoja.
Ufoo Saro hakuweza kuhudhuria mazishi ya mama yake manake bado anaendelea kupata matibabu ya risasi mbili alizopigwa na Mwanaume ambae baadae nae alijiua akijua amewaua mama Ufoo na Ufoo mwenyewe.
No comments:
Post a Comment