New York mission of Tanzania yaadhimisha siku maalumu ya kumkumbuka na kumuenzi Mwl Julius Kambarage Nyerere. Maadhimisho hayo yalifanyika kwa mara ya kwanza ndani ya ECOSOC Chamber, ukumbi uliopo ndani ya jengo la UN hapa New York na kuwakaribisha mabalozi mbalimbali wawakilishi wa Umoja wa Mataifa. Mabalozi hao walipata fursa ya kutoa wasifu wa Mwl Nyerere kutokana na mambo aliyoyafanya kipindi cha uhai wake kimataifa. Licha ya kuadhimisha siku hii maalumu, kilizinduliwa kitabu kinachoelezea historia ya maisha yake na mambo muhimu aliyoyafanya kipindi cha uhai wake. Kitabu hicho kimeandikwa na kuhaririwa na Profesa Ali Mazrui pamoja na Linda Mhando na kuuzwa hapohapo ukumbini. Baada ya kutoka hapa kulifuatiwa na chakula na vinywaji ndani ya ukumbi wa Tanzania Mission.
Profesa Mazrui akitia sign kwenye kitabu baada ya watu kukinunua
Balozi wa India na Balozi Mwiny wa Tanzania wakiwa ndani ya ukumbi huo
1 comment:
Bongolala tunaletewa zilipendwa tucheze ili tuachane na kiduku (rasimu ya katiba) kwa muda!! Kama kawaida mambo ya upepo!!
Post a Comment