Advertisements

Thursday, October 3, 2013

MWANAMKE ALIMANUSURA AVUNJE GETI JUMBA JEUPE KWA OBAMA, AUWAWA BAADA YA KUKIMBIA


Mwanamke anayekadiriwa miaka 34 Mmarekani mweusi akiwa na mtoto anayekadiriwa umri wa mwaka mmoja, leo mchana akiwa na gari aina ya Infiniti nyeusi ya mwaka 2005 alijaribu kuingia kwenye geti la White House kwa Obama kwa kuligonga aliposimamishwa na police wa Capitol alikataa kutii amri na kuondoka kuelekea kwenye mjengo wa Capitol Hill kujaribu kuingia mjengoni humo huku akifukuzwa na magari ya Polisi na yeye kuendelea kukaidi amri ya polisi baadae aliuwawa baada pia  kumgonga polisi ambaye kwa sasa anaendelea vizuri pamoja na mtoto wa mwanamke huyo.

Gari ya mwananke huyo iliposachiwa haikukutwa na silaha yeyote wala milipuko na mpaka sasa hizi polisi hawajui ni kwanini mwanamke huyo alijaribu kufanya hivyo lakini uchunguzi wa awali unasema mwanamke huyo alikua na matatizo ya akili na pia Polisi wamekataa kutaja jina lake na sasa hivi wapo kwenye nyumba yake jimbo la Connecticut wakijaribu kutafuta kama wanaweza kupata sababu ya mwanamke huyo kujaribu kuingia White House na Capitol Hill.

Habari nyingine  inayoendelea kuwa gumzo kwenye vyombo vya habari ni ile ya kusitishwa kwa shughuli zote za kiserikali na leo ni siku ya tatu tangia Rais Barack Obama alivyotangaza siku ya Jumatatu. Bado muafaka haujafikiwa na pande zote mbili na Rais Obama amesema hataki mazumuzo kuhusu mswada huo wa afya unaojulikana kama Obama Care.

Wadadisi wa mambo wanadai upande wa upinzani wanafanya makusudi kwa kutoupitisha mswada huo kwa madai kwamba hauwanufaishi wananchi, madai ambayo Rais Obama anasema sio ya kweli.

No comments: