ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, October 6, 2013

NAWASHUKUNI SANA WATU WOTE !!!!!!!!!!!

Nafasi ya kwanza kwa shukurani zangu inakwenda kwa yeye aliyeumba mbingu
na nchi, Mungu wetu yeye ambaye NIKO. Jambo la msiba lililokuwa katikati 
yangu na familia yangu nyumbani Tanzania ni kama moto uunguzao nafsi,lakini
Mungu ametufariji sana hata tumemaliza msiba vyema hapa USA na Tanzania.

Nafasi ya pili inakwenda kwa Wachungaji wote wa DMV [ Rev's John Kadyollo,
John Mbata, Ferdnand Shideko, Melkizedeck Maturu, Augustus Baraza, Peter
Igogo, Samson Ananiah na Stella Swai ] wote Mungu awabariki sana kwa kuja 
nyumbani kwangu na kanisani kuniombea na kunifariji mtumishi mwenzenu. 
Mungu awabariki sana watumishi.

Nafasi ya tatu inakwenda kwa uongozi wa jumuiya ya Watanzania NY  na DMV kwa
kunipigia simu kwa kunipa pole na kunitia moyo. Mungu akubariki sana mwenyekiti
wetu Idd Sandali kwa kuja kunitia moyo wa faraja na neno ulilotoa mbele ya watu 
waliohudhuria kwenye misa leo tar.10/5/2013 - Mungu akubariki sana ndugu yetu.

Nafasi ya nne inakwenda kwa dada zangu wapendwa kwa kuwa pamoja nami ktk
kipindi hiki kigumu na kutia moyo wa faraja kuu. Mungu akubariki sana dada zangu
Beaty Lulandala, Faith Isingo, Hilda Kivembelle, Lizzy Luhanga, Pamella Luhanga,
Rukia Malipulla, Terri, Leah Nyaki na Cleopatra. Tena na tena, Mungu awabariki.

Nafasi ya tano inakwenda kwenu wadogo zangu, James Kivembelle na Jeff Deo Nkanda
Nanyi pia Mungu awabariki sana kwa kuacha kazi zenu na kuja kunifariji. Pia akina shemeji
 popote mlipo Mungu awabariki sana kwa kuwa pamoja nami na kuwaruhusu
dada zangu kuja kwenye shughuli za msiba tangu mwanzo hadi mwisho.

Asante sana Bro. Katanga, Ellias Mshana, Neema Babu na familia yako, Mshama
family, Familia ya Mr & Mrs Lawa, Familia ya Raymond A, Mr Titus Mazalli, Bi
Fatma, Familia ya Taji, Ndugu yangu Kingalu [ Kenyatta ], nyie wote pokeeni hizi
shukurani zangu na baraka toka kwa Mungu aliyemuumba wetu kwa kuja kuniona
na kunifariji. Siku ile Bwana Yesu atasema hivi," Nalikuwa ktk huzuni mkaja kuniona"
 
Nanyi nyote mpatao jumla yenu 218 mlionipigia simu toka Tanzania, Buffalo NY,
Montrial Canada, Fabiossy Family of Brazil, na UK. Mliotuma text msg 91 kwa simu
zenu za mkononi na voice mails, Mungu awabariki sana kwa moyo wenu. Endeleeni
kusoma vijimambo blog zaidi ya mara tatu kwa siku ili kupata habari mbali mbali.

 Mwisho nawashukuru watoto wa kiroho Lilian Semiti, Iman Abdu, Lilian Mzava,
Familia ya Neto na Kate, Mama Mungu [Edna Mushi ], Adonai Fellowship wote
pamoja na kanisa la Assemblies of God - Silver Spring.......Nyote Mungu awabariki. 

NB: ASANTE SANA MKUU, DJ LUKE JOE KWA YOTE HASA KWA KUIHA-
      BARISHA JAMII YA WATU WANAOONGEA KISWAHILI HAPA DUNIANI.
Nilipigiwa simu nyingi sana toka nje ya USA sababu yako Vijimambo - Mungu akuba-
sana kwa kazi njema. Sikupendelei bali nasema ukweli kuhusu kazi zako kwa jamii.

na wote ambao sikuwata hapa leo Mungu awabariki sana kwa kuniombea na kujumuika
nami katika kipindi kigumu cha kufiwa na mama mpendwa.

Mch. Malekela MJ - Kanisa la Assemblies of God, Silver Spring MD.

No comments: