Juma Omolo Swaga, 80, (kushoto) na John Akula Swaga, 89 (kulia)
Ndugu mmoja alipatwa na fikra za kwamba ndugu yake ameshafariki dunia baada ya kupotea kwa miaka 70 lakini kumbe bado anaishi. Mzee Juma Omolo Swaga mwenye miaka 80 alipoteana na kaka yake John Akula Swaga mwenye 89 ndani ya miaka 70 iliyopita. Kipindi hicho Juma Omolo alikuwa na miaka 10 na kaka yake alikuwa na miaka 19. Juma aliondoka na dada yake kwenda kutafuta vibarua kwenye mashamba ya wakoloni nchini kwao Kenya na baadaye aliendelea na maisha bila kuwasiliana na nyumbani kwao.
Baadae maisha yalimpereka hadi Uganda maeneo ya Subukia ambapo alikaa huko kwenye miaka ya 1970. Ndugu yake alipata habari kwamba mdogo wake amejiunga na jeshi la Idd Amin na kufariki kwenye vita. Kumbe hizo habari hazikuwa za kweli. Kaka yake anasema,”Hata marehemu mama yetu alienda kumtafuta Juma huko Uganda lakini hakumpata, lakini leo nimejua kuwa ni yeye kwasababu ana kovu ambalo ni la kudumu na bado analo hadi leo.”
Juma Omolo anaogea lugha ya Kikuyu vizuri kabisa ambayo ndiyo lugha ya asili ya kwao licha ya kukaa nje ya huko kwa muda wa miaka 70. Kaka yake alipokea barua kutoka kwa chifu wa eneo lao ikimuambia kwamba mdogo wake amefika maeneo ya Nakuru na anawatafu
ta.

No comments:
Post a Comment