ANGALIA LIVE NEWS

Monday, October 7, 2013

NYENZO ZA MADJ WA ENZI HIZO


Cassette aina ya Metal

Cassette aina ya METAL  ilikua ni moja ya Madj wa enzi hizo kama Tajiri mtoto (young Millionaire) Dj Paul Mac G, Dj Super Deo, Dj Gerald, Dj Seydou, Dj John Pantalaksi, Dj Joseph Kusaga, Dj Joe Jonson, John Kitambi, Dj Chris Phaby, Dj Deo Composer, Dj Junior Challenger, Dj Agip Show, Dj Nigga Jay na maDj wengine waliotangulia mbele ya haki kama Dj Kalikali, Dj David Joseph, Dj Clement, Dj Roma Pop Juice, Dj Choggy Sly na wengine wengi walielewa ubora wake wa kurekodi muziki na ukatoka bomba sana na kutokana na Cassette aina hiyo kutokupatikana Tanzania Enzi hizo au kama itatokea kupatikana basi bei yake ilikua ghali kwa Dj kuweza kuimudu. Na Cassette ya metal ukisha kurekodi muziki mara nyingi walishauri kutoirekodi tena kutokana na ule muziki wa uliorekodiwa mwanzo bado utaendelea kusikika kwa mbali.

Chrome ni aina nyingine ya Cassette iliyokuwa ikitoa muziki mchicha sana, na Normal kama jina lilvyo muziki wake ulikuwa wa kwaida.

Cassette aina ya Chrome

Mara nyingi upatikanaji wa muziki enzi hizo ulitokana na mabaharia waliorudi likizo na  au wazazi wa watoto waliokua wakisafiri kikazi na muziki wakati mwingine ulipatikana kutoka kwa wasomi vijana waliomaliza masoma au kurudi likizo. Upatikanaji wa muziki huu Madj wengi walitumia jina la kunyonya au kufyonza wa kimaanisha kurekodi.


Tukirudi kwenye Cassette kulikua na aina zaidi ya tatu na zilizofahamika sana zilikua Normal, Chrome na Metal. Cassette ya Chrome na Metal ndio ilikuwa ikikupatia muziki uliorekodiwa kutoka mchicha tofauti na cassette aina ya Normal na tofauti ya Chrome, Metal na Normal ilikua rangi ya tape yenyewe (utumbo) Chrome na Metal utumbo wake ulikuwa mweusi na Normal ulikuwa kahawiya pia aina hizo za cassette zilitofautiana urefu zingingine 60, 90 na 110 namba hizo ziliashilia cassette inaweza kucheza muda gani na Madj wengi walipenda urefu wa dkk 60 kutokana na ule mrefu mara nyingi huleta matatizo ya kujikunja utumbo au mpaka kunasa kutokana hali ya joto ya Dar es Salaam ilvyokuwa na Madisco mengi kutokuwa na viyoyozi kutokana na kumbi nyingi kuwa wazi katikati.

Cassette aina ya Normal

Kutokana na watu wengi kutokuwa na uelewa wa utofauti wa utumbo wa aina hizo tatu za cassette, Madj wengi walitumia mwanya huo kubadilisha utumbo wa cassette utakuta Dj kapewa Chrome na mteja wake amurekodie nyimbo badala yake dj atarekodi nyimbo kwenye cassette ya normal na kuifungua na kubadilisha utumbo na kuweka utumbo wa Normal kwenye cassette ya Chrome. Tabia hii ilifanywa sana na Madj wa zamani na kama atamkuta mteja anaelewa tofauti na utumbo wa chrome na Normal basi litatibuka timbwili si la kawaida.

Yote hayo yalifanywa na Dj bila hata yeye kuwa na uelewa kwamba Cassette Player ziliwezakutambua aina ya cassette inayochezwa kutokana na matundu yaliyopo juu ya mgongo wa cassette. Cassette aina ya Normal ilikua na matundu mawili kwenye engo mbili za mwisho kwenye mgongo wa cassette hiyo, cassette aina ya Chrome ilikua na matundu mawili engo za mwisho kwenye mgongo wa cassette hiyo tofauti yake na cassette ya normal matundu yake yalikuwa mapana na cassette ya Metal ilikuwa na matundu kama ya chrome na matundu mengine madogo mawili katikati ya mgongo wa cassette yenyewe.

Matundu hayo ndio yaliweza kuifanya Cassette player kutambua ni aina gani ya cassette inayocheza. Kama kasha ni Normal na utumbo ni chrome bado cassette haitatoka mchicha kamailivyotarajiwa.

Kitu kingine kilichochangia cassette kutotoa muziki mchicha ni brashi iliyopo juu ya cassette katikati kama brashi itaenda upande au itakuwaimetoka kwa bahati mbaya basi ujue muziki wako hautatoka ipasavyo. Kitu kingine ambacho Mdj wengi walikuwa hawakifahamu ni kichwa cha cassette player kinapochafuka kutokana na cassette kuachwa nje ya makava yake na kusababisha brashi kushika vumbi na unapocheza kwenye cassette player vumbi inabaki kwenye kichwa cha cassete player hiyo na kusababisha muziki kutokua mchicha na kitu cha mwisho ni uishaji wa kichwa cha cassette player mara nyingi kinapotumika sana inafikia wakati wa kukibadilisha.

No comments: