Ndugu Zetu Watanzania Wote,
Tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa ushirikiano na upendo wenu mkubwa kwenye Ziara nzima ya Ommy Dimpoz hapa Marekani. Kusema kweli tumefarijika na kufurahishwa sana na kujitokeza kwenu kwa wingi ili kuhakikisha tunafanikisha shows kwa kiwango cha juu. Inatia moyo sana kuona jinsi Watanzania tulivyoungana na kuwa kitu kimoja kwenye ziara hii. Kutoka Washington DC mpaka Los Angeles mlijitokeza kumtia joto Kijana wetu Ommy Dimpoz na kwa hilo tunashukuru sana. Mwisho tunapenda kuwaomba radhi pale ambako kulitokea mapungufu na tutaendelea kujitaidi kuboresha na kufanyia kazi kasoro zilizojitokeza. Tunaomba tuendelee na Moyo huo huo kwani silaha yetu kubwa kama Watanzania ni umoja wetu. Tunawatakia kila la kheri kwenye shughuli zenu za kila siku na Mwanyezi Mungu azidi kuwabariki na kuwapigania.
Wenu,
Ligate na Dickson Mkama - Waandaaji wa Ommy Dimpoz Nai Nai US Tour

2 comments:
Wewe dmk kurembua macho ni pozi au maringo?
Wewe dmk kurembua macho ni pozi au maringo?
Post a Comment