ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, October 8, 2013

TAARIFA YA MSIBA NEW JERSEY NA TANZANIA

Waheshimiwa Wanajumuiya,

Tunasikitika kutoa taarifa kwamba Bwana Joseph Maige wa New Jersey amefiwa na kaka yake Godwin Maige aliyefariki huko Nairobi, Kenya alikokuwa akipata matibabu. Taarifa hizi zilitufikia jana jioni.

Tunawaomba wote tuwe pamoja katika kuomboleza msiba huu. Joseph atapatikana nyumbani kwake New Jersey Jumatano tarehe 9 na Jumapili tarehe 13 Octoba (wiki hii), kuanzia asubuhi mpaka jioni. Hivyo mnaweza kufika kumpa pole na kuomboleza muda huo. Anwani yake ni: 261 Bergen Avenue hapo New Jersey. Na simu yake ni 201-702-0342.

Ibada ya kumwombea marehemu itafanyika baada ya siku arobaini na taarifa zaidi zitafuata baadae.

Tunawaomba wanajumuiya tuomboleze pamoja na ndugu yetu Joseph Maige.

Tunawashukuru kwa ushirikiano wenu.

Raha ya milele umpe ee Bwana na mwanga wa milele umwangazie, apumzike kwa amani. Mungu aiweke roho ya marehemu Godwin Maige mahali pema peponi. Amina.

Kwa niaba ya jumuiya,

Deogratius Mhella
The Executive Secretary
New York Tanzanian Community
c/o Tanzania Mission to the UN
201 East 42nd. Suite # 425
New York, NY 10017
Email: info@nytanzaniancommunity.org

No comments: