ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, October 9, 2013

Tukio la ajabu la mganga kuchukua milioni kadhaa kumfufua mtu Geita, stori yake iko hapa


Unaambiwa kwenye wilaya ya Geita Mwanamke mganga wa kienyeji aitwae Hamisa Benjamin mwenye umri wa miaka 26 mkazi wa kijiji cha Katoro, ilibaki kidogo tu auwawe na Wananchi baada ya kushindwa kumfufua mtu.

Hili tukio limetokea siku kadhaa baada ya Polisi kwa kushirikiana na Wataalamu kutoka ofisi ya mkemia mkuu kanda ya ziwa, kufukua kaburi linalosadikiwa kuwa na viungo vya mtoto Shaban Maulid mwenye umri wa miaka 15 aliefariki miaka mitatu iliyopita alafu ikadaiwa ameonekana akiwa hai hivi karibuni.
Marehemu wa hili tukio la Geita ni Mbelwa Lukaza ambapo kutokana na kifo chake cha ghafla chanzo kikiwa ajali ya gari August 28 2013, mkewe aitwae Tausi alikwenda kwa mganga huyu wa kienyeji na kuhakikishiwa kwamba mume hajafa hivyo uwezo wa kurudishwa na mganga huyu upo.

Tausi anasema ‘kifo cha mume wangu kilinisikitisha ndio maana nikaja kwa mganga kwa sababu aliniambia anauwezo wa kumrudisha mume wangu, nilikua bado kwenye msiba hivyo nikawaambia na wifi zangu tukakubaliana wote na kuja hapa kwa mganga, tukaambiwa mtu wenu yupo tutamvuta ila mtoe kwanza laki tatu…. alivyoendelea kumtibu Mganga akasema mgonjwa wenu ameharibika sijui Macho,Pua, sehemu za siri, mnatakiwa mtoe hela zaidi…. baada ya siku mganga akasema sasa mmemaliza kabisa, ulimi ndio wa mwisho’

Unaambiwa baada ya Marehemu kushindwa kufufuliwa, ndugu na marafiki walimtaka mganga arudishe pesa zote alizolipwa zinazokadiriwa kuwa zaidi ya shilingi milioni 5 ambapo Hussein Nasoro akiwa kama ndugu anasema ‘tulichoka kusubiria kwa zaidi ya mwezi mmoja, mama alikua anakwenda nyumbani anachagua vyombo… mganga anasema mgonjwa anaomba sehemu ya kukalia, godoro la kulalia, mayai na maziwa… sasa hivi vyote tulimpa mganga na tulipoingia kwake tumeviona vitu pembeni ila mgonjwa hayupo’

‘Tumepoteza zaidi ya milioni 5, gharama za kusafiria kufatilia hati za viwanja… dawa na mengine! hiyo yote tulifanya kwa sababu tulitaka kufanikisha swala la kumpata huyu mtu kama tulivyoambiwa kwamba yupo japo tulishamzika na tuliamini amekufa’ – Nasoro

Mganga Hamisa ambae anashikiliwa na polisi baada ya kunusurika kuuwawa kwenye fujo zilizodumu kwa saa kadhaa, amekiri kuahidi kumfufua marehemu ambae kwa sasa anasema hayuko tena, ametoroka kutokana na kelele na vurugu zilizokua zinafanywa na ndugu na jamaa.

No comments: