ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, October 9, 2013

Yote aliyoyasema Mzee Majuto kuhusu kugombea Ubunge 2015


Mwigizaji Mzee Majuto ameingia kwenye headlines baada ya kufanya interview na host wa Amplifaya yaClouds FM na Clouds FM Top 20 Millard Ayo na kuongea kuhusu mpango wake wa kugombea ubunge kwa mara ya kwanza mwaka 2015.

Majuto ambae makazi yake ni 96.0 Tanga anakwambia ‘kama Mwenyenzi Mungu atanifikisha umri huo, mwaka 2015 nitagombea Ubunge kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa sababu na wenzetu mbona wamegombea na wamepata kina Sugu nao ni wasanii wamepata na wanafanya vizuri’
‘Lengo langu ni kuwa karibu zaidi na jamii, ndivyo nchi inavyotakiwa kuendeshwa… nalifahamu jimbo langu la Tanga na matatizo yake yakiwemo umeme, maji na ardhi, na huenda nikagombea Tanga Mjini ila ikishindikana kwa Tanga mjini nitakwenda kugombea kwenye wilaya ya Mkinga’ – Majuto

‘Hii nchi nimetembea sana, ninacholilia ni ardhi ambayo nimekutana nayo… mipori kwa mipori kwelikweli lakini sio ya hifadhi, vitendea kazi vimekua tatizo manake Muheshimiwa Rais amejitahidi kutafuta Matrekta akisema watu wawe kwenye makundi ili wafanye kilimo lakini watu hao wakishapewa Trekta kuna ujanjaujanja na ubabaishaji wa wasimamizi mwisho hakuna kinachofanyika’ – Majuto

Kingine alichosema atakishughulikia Mzee Majuto ni viwanja vinavyogawiwa na Serikali Tanga, anasema kumekua na ubabaishaji mkubwa na ni watu wachache sana wanaopewa kihalali, viwanja vingine vinachukuliwa kwa dili kuchezwa alafu badae vinakuja kuuzwa bei ghali.

Mzee Majuto ambae wazazi wake wote ni wazaliwa wa 89.2 Kigoma, ana umri wa miaka 65 na idadi ya watoto wake ni 9 ambao saba kati yao amewapa ajira kwenye utengenezaji wa filamu zake za vichekesho… akiwemo Cameraman, dereva, meneja, waigizaji na mpishi…

1 comment:

Anonymous said...

Sasa nimeanza kututania wananchi wa-Tanzania naona!!! Mtu hata kujieleza hawezi kabisaaa atagombaniaje ubunge???? Watanzania tusipo kuwa makini na viongozi tunao wawekezaji madarakani tuts endelea kuwa wa Mwisho tu Kila pahali!!! Si waigizaji Woote wana weza kuwa madaktari na pia si madaktari Woote waweza kuwa waigizaji-Akili kumkichwaaa!