Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Ramadhan Mwinyi akizungumza wakati wa mkutano uliokuwa ukijadili kuhusu Maendeleo ya Jamii, na mkazo mkubwa ukisisitizwa katika maendeleo endelevu yanayojumuisha makundi yote likiwamo kundi la Wazee. Akizungumzia uzoefu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika utekelezaji wa sera na mipango mbalimbali inayolenga kuwapatia unafuu wa maisha wazee, Balozi Mwinyi alieleza kwamba kwa kutambua mchango mkubwa wa kundi hilo la Jamii , Tanzania licha ya changamoto mbalimbali imejiweka sera na mipango inayojikita katika kutoa unafuu wa maisha kwa wazee. Akazitaja baadhi ya huduma hizo kuwa ni pamoja na huduma za afya na makazi kwa wazee wasiokuwa na uwezo.
No comments:
Post a Comment