Ukipewa Msaada wa kubebwa mgongoni,usianze machejo ya kumtekenya aliyekubeba,atakuangusha bure..
Hii ni kwa wale WANAUME wasio na Shukrani..Unajijua kabisa huna Mvuto na Sura yako haina haiba,kwa kifupi una Sura la Mjomba kama bata mwenye mdondo lakini Mungu sio Mrishp Ngasa,kuna mdada wa watu bila kujali muonekano wako hafifu na duni,amejitoa Kimasomaso kukupenda kwa dhati japo huna Sura wala huna hela na hadhi ya kuwa na msichana kama huyo.Mdada wa watu anajitahidi kujilinda,anakwepa vishawishi vya Mapedeshee wa town ambao wanahonga kuliko kutoa sadaka kanisani,anakataa Ma-handsome boy kibao wanaomtaka,kwa sababu yako.Badala ya kushukuru na kulipa wema,angalau na wewe anakuweka mjini unaonekana unamiliki mzigo wa maana,unaonekana nawe umo wewe ndo umekuwa Fungulia-Mbwa,Unamcheat waziwazi
Sasa hivi unajiona mjanja kwa sababu yupo,na unajua anakupenda ila siku moja atakuchoka atakuacha,Sasa Sijui utapata wapi mdada mwingine wa kujitoa Mhanga kukupenda na sura lako kama umepewa taarifa ya Msiba.
Heshimuni Wadada wa watu wakijitoa kuwapenda kama mlivyo...Nakushangaa sana wewe Kijana unapata wapi Ujasiri wa kuleta mawenge kwa huyo mdada wakati unajua kabisa Hela huna na una sura kama Bonde la Ufa.....UKISITIRIWA BASI UJUE KUSITIRIKA.

2 comments:
safi sana sijajua wakina baba wanabeba watoto huko bongo imekaa poa ile mbaya mambo safiiiiiiiiiiiii bongo kama majuu
E bwana mpwa huyu mtu aliyeandika hiki kibwagizo cha maonyo ni mtu muhimu sana kwa kuichonga na kuirekebisha jamii ya vijana ambao kila leo chupi mkononi bila kuwajali wake/wapenzi wao. Ni kweli akina dada walio wengi mwanangu ni visura sana lakini sisi akina kata k noma sana. Tena bila aibu unamuacha mrembo wa ujana wako na watoto 2, 3 au zaidi kisa anakuuliza kwanini unarudi usiku. Ama akikuuliza mbona unafanya kazi masaa 4 tu kwa siku wakati kimwana wako anapiga 16 tena weekend zote, wewe umechagua kukaa na watoto kwenye park na kuchati na vibaka. Safari haziishi kibaka weeeee, mara NY, AL, CA nk.
Post a Comment