ANGALIA LIVE NEWS

Monday, October 28, 2013

UZINDUZI WA TAWI LA CHADEMA LA OHIO ULIOFANYIKA COLUMBUS JUMAMOSI

Viongozi wa tawi la CHADEMA DMV wakiwa na wenzao wa CHADEMA OH siku ya ufunguzi wa tawi uliofanyika jumamosi Oct 26, 2013 mjini Columbus, Ohio.
Kiongozi wa tawi CHADEMA OH akiongea sababu zilizopelekea na kuamua kufungua tawi la CHADEMA Ohio pia alitumia muda huo kuwakaribisha viongozi wa tawi la CHADEMA DMV ambao walikuwepo kushuhudia uzinduzi huo.
Mwanyekiti wa CHADEMA DMV akiongea machache kwa kuwapongeza Watanzania wa Ohio kwa muamko wao na kuamua kufungua tawi la CHADEMA OH ili kuleta mawazo mbadala yatakayoweza kuikomboa nchi yetu.
Katibu wa CHADEMA DMV akitoa shukurani zake kwa ukaribisho alioupata yeye na msafara mzima kutoka DMV pia alitumia muda huo kuwapongeza CHADEMA OH kwa maamuzi yao ya kufungua tawi CHADEMA OH na kuwataka Watanzania wengine waliopo majimbo mengine waige mfano wa Ohio, huku ni kukomaa na kuwa na uchungu na Tanzania.
Mwenyekiti wa CHADEMA DMV akikata utepe kuashiria tawi la CHADEMA OH limefunguliwa rasmi
Mwenyekiti CHADEMA DMV akilishwa keki na kiongozi  wa tawi CHADEMA OH
Ilikua ni wakati wa kulisakata Rhumba
Picha na Akili Mtaalam,
kwa picha zaidi bofya sooma zaidi

4 comments:

Anonymous said...

magwanda hata kwenye muziki?

Anonymous said...

Huyo benja mikutano ya chedema upo ya ccm hauji wewe vipi ??

Anonymous said...

1. Wabongo bwana wanachojua ni majungu tu. Kwani kuna sheria inayosema watu wasicheze muziki na gwanda? mbona wakicheza muziki na gamba husemi????!!!

2. Alichoonyesha BENJA ni ukomavu wa kisiasa, kwa sababu mkutano huo ulialika watanzania wote bila kujali itikadi zao. Sasa wewe uliekerwa na hilo pole. Long live Benja. Long live people's power. Congrats Columbus, Ohio

Anonymous said...

Jackson lyimo Mara CCM mara Chadema.mtoto wa mzee kimambo kiboko