Naibu katibu mkuu wa CCM na mbunge wa Iramba magharibi Mwigulu Nchemba alifanya ziara hivi karibuni jijini Washington Dc na alizungumza na watanzania pia alipata nafasi ya kutembelea idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Amerika(VOA). Katika mahojiano yake na Kipindi cha Matukio Afrika pamoja na mambo mengine alielezea kazi za chama chake na suala la elimu nchini Tanzania
Kuhusu suala la shutuma za kushuka elimu nchini humo alisema "tatizo la waafrika tunapima uwezo wa wanafunzi kwa kutumia lugha" aliongeza kuwa wanafunzi wanao uwezo ila hawapati nafasi ya mafunzo ndani ya kazi yaani nadharia kwenye maeneo ya kazi.
Aidha alipoulizwa kuhusu suala la kusafiri na mshauri wa rais amesema ni kwa kuokoa gharama na kuwaita kwenye mkutano wa vyama katika muda wake wa ziada na amechukuliwa kwenye mkutano wake na chama kinamgharamia kwa yale yasiyohusisha serikali aliongeza.
Kusikiliza mahojiano hayo bofya hapa.
http://www.voaswahili.com/archive/matukio-afrika/latest/2773/3100.html

2 comments:
Huyu Mwigulu anakifahamu anachokiongea ? Sasa kama lugha ya kujifunzia ni kiingereza yeye anataka wanafunzi wapimwe kwa kiswahili? Mbona Kenya na Uganda ni tofauti na anachokiongea? Ukweli ni kwamba English ni tatizo kubwa Tanzania peke yake... Mkiambiwa mitaala mibovu mnabisha :( sasa technology yote ni ya kuazima kwa wazungu unategemea tupime wataalamu kwa kiswahili? Kama tatizo ni nadharia si niserikali yako ya CCM iliyosahau kuwekeza kwenye elimu!! Mbona unatuchanganya? South ,West Africa wote wanatumia English kama lugha ya kwanza sasa ni wapi Africa ambako English ndiyo kigezo cha uwezo wa mwanafunzi kama siyo bongo? Unaongea bila research?
jamami msiharibu lugha yetu ya kiswahli viingereza ndo nini tena,kama kweli ni waandishi wa habari au watoa habari basi kuweni na utaalamu wa kuandika vizuri hakuna kitu kinachoitwa viingereza kama ndo madoido basi punguzeni siyo bongoflava hii
Post a Comment