Nassoro Basalama akiongea jambo na Mshobozi Kamugisha kabla ya kuanza kurekodi kipindi cha Kijiwe cha Ughaibuni na wadau wa North Carolina, Oct 26, 2013 Kruu ya Kijiwe cha Ughaibuni watakuwa New York.
Edna Ntirugelegwa akiandaa makulaji kwa kruu ya wanaKijiwe mara tu ilipowasili Durham, North Carolina kwa ajili ya kurekodi kipindi cha Kijiwe cha Ughaibuni wiki ijayo.
Wanakijiwe wa North Carolina wakirekodi kipindi chao kuhusu kushuka kwa Elimu Tanzania na nini kifanyike kuboresha mfumo wa elimu kwa ujumla pia walizungumuzia tattizo la msongamano jiji la Dar es Salaam na nini wanachofikiri kinaweza kuwa ufumbuzi wa tatizo hilo. Washiriki waliorekodi kipindi cha Kijiwe cha Ughaibuni walikuwa David Mushi, Nassoro Basalama, Elizabeth Kyangenyerika, Tony Mtirungelegwa, Edna Ntirungelegwa, Kwiti Kamugisha, Mshobozi Kamugisha, Agneta Kamugisha na Geofrey Lepana.
Mpwa katika picha ya pamoja na Mwana Njenje ambaye ni mmoja ya wawakilishi wa Vijimambo North Carolina.
Kruu ya Kijiwe cha Ughaibuni inatoa shukurani za dhati kwa washiriki wote waliojitokeza na ambao hawakuweza kufika kutokana na majukumu japo nia ilikuwepo.
Shukurani za pekee kwa dada yetu Edna Ntirungelegwa kwa mapishi yaliyoenda skuli kusema ukweli Kruu ya Vijimambo haina cha kukulipa kitakacholingana na ulichokifanya umetumia muda wako ambao ungeweza kuutumia kwenye shuguli za kipato kusema ukweli upendo na ukarimu wako ni mfano wa kuigwa.
Shukurani zingine za pekee zimwendee kaka yetu Geofrey Lepana kwa msaada wako kwa Kruu ya Kijiwe asante sana na Mwenzezi Mungu akuzidishie mara mbili ya hayo. Wema na upendo wako ni mfano wa kuigwa na jamii inayokuzunguka na Watanzania wote waishio ughaibuni.
2 comments:
mwana njenje ndo huyu aliyetoga mazikio na kufaa vipuri au? jijuzeni wadau ha ha ha amakweli dunia inamambo na marekani kiboko ha ha ha
safi sana sana wakina mapaje na yassin watakula kwao ndo inavyotakiwa hivyo wakinuna watu nendeni kwengineko ambapo watu hawana mambo ya kijinga jinga. safi sana crew yote ya kijiwe cha ughaibuni
Post a Comment