


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Dkt. Emmanuel Nchimbi akitoa hotuba ya ufunguzi kwa wajumbe wa Mkutano wa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza( hawapo pichani) katika Ukumbi wa Hoteli ya Edema, Mkoani Morogoro. 

Baadhi ya Wajumbe Washiriki katika Mkutano wa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakisikiliza hotuba ya Mgeni rasmi(hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza katika Ukumbi wa Hoteli ya Edema, Mkoani Morogoro. 

Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi, Mhe. Dkt. Emmanuel Nchimbi( wa nne kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza kwa waliosimama katika picha mara baada ya kufungua rasmi Mkutano huo leo Oktoba 23, 2013 wa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza utakaofanyika kwa siku mbili katika Ukumbi wa Hoteli ya Edema, Mkoani Morogoro( kushoto kwa Waziri) ni Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mbarak Abdulwakil( kulia kwa Waziri) ni Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja. Wengine ni Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Haji Janabi(wa kwanza kushoto), wa pili kushoto ni Kamishna wa Huduma za Urekebishaji, Deonice Chamulesile(wa tatu kulia) ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa na wa pili kulia ni Kamishna wa Fedha na Utawala, Gaston Sanga. Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza.
No comments:
Post a Comment