Saturday, November 23, 2013

Balozi Sefue akutana na Mkuu wa Taasisi ya Uongozi ya China

Makamu wa Rais wa Taasisi ya Uongozi ya Jamhuri ya Watu wa China Mh.Hong Yi akimkabidhi nakala ya kitabu chenye nasaha za watu mashuhuri kutoka jamhuri ya watu wa China Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue ikulu jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mkuu wa Taasisi ya Uongozi Tanzania Profesa Joseph Semboja. Awali viongozi hao wawili walifanya mazungumzo yenye lengo la kuimarisha uhusiano kati ya Taasisi ya Uongozi ya China na ile ya Tanzania.Taassisi hizo mbili zinatarajia kutia saini mkataba wa ushirikiano wiki hii.

Taasisi ya Uongozi Tanzania(Uongozi Institute pamoja na Taasisi ya Uongozi ya China(Chinese Academy of Governance) zinatarajiwa kusaini Mkataba wakukuza ushirikiano kati ya taasisi hizo mbili Jumanne wiki ijayo jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Taasisi ya Uongozi Institute Profesa Joseph Semboja ameyasema hayo jijini Dar es Salaam leo baada ya Ujumbe kutoka Taasisi ya Uongozi wa China( Chinese Academy of governance) kumtembelea Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue ikulu jijini Dar es Salaam.

Ujumbe huo kutoka Jamhuri ya Watu wa China unaongozwa na makamu wa Rais wa Taasisi hiyo Bwana Hong Yi na ziara hiyo inafuatilia ziara ya hivi karibuni ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda ambayo pamoja na mambo mengine uhusino kati ya taasisi hizo mbili ulitiliwa mkazo.

Profesa Semboja aliongeza kusema kuwa mkataba wa mahusiano kati ya taasis hizo utawezesha ubadilishanaji wa teknolojia na utaalamu na hivyo kuboresha mafunzo yanayotolew na taasisi ya Uongozi Tanzania.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue alimshukuru Bwana Hong Yi kwa nia yake njema ya kushirikiana na Taasisi ya Uongozi Tanzania na kuongeza kuwa ushirikiano kati ya China na Tanzania ni wakihistoria na wenye manufaa makubwa kwa wananchi wa nchi hizo mbili.
Katibu Mkuu balozi Ombeni Sefue akiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais wa Taasisi ya Uongozi ya China Mh.Hong Yi ikulu jijini Dar es Salaam leo(picha na Freddy Maro)

No comments: