Wednesday, November 20, 2013

CANNIBAL ALA VICHWA VITATU TU SHOW YA UARABUNI, SI ALIJITAKIA HUYU MUSIC WA AINA YA HIP POP UKAFANYE SHOW UARABUNI WENZIO WALA BATA WEWE UWAPELEKEE SAMAKI

Legend rapper kutoka chini Kenya aliyekuwa ndani ya kundi la Ukoo Flani maarufu kama Cannibal Shattah, amepatwa na kituko cha mwaka, ikiwa ni siku chache tokea rapper huyo atoe video clip ya yeye akiwa Dubai ana-ball hard kama wanavyosema vijana wa siku hizi na kumjibu rapper wa Kenya, Prezzo kuwa yeye ni legend na ana hela za kutumia.
Cannibal ambaye ameenda uarabuni (Dubai) kupiga show alipatwa na mkasa mkubwa ambapo alipata fans watatu tu katika ukumbi mzima alipoenda kupigia show hiyo, pia rapper huyo alishikiliwa airport Dubai kwa kuhisiwa kuwa amebeba madawa ya kulevya (Narcotics) kwa muda wa masaa tano.

Promoter wa msanii huyo amechukizwa sana na watu wa Kenya kwa kusambaza habari za kinafiki na kufurahishwa na mkasa uliomkuta msanii huyo na kusema kinachotakiwa ni kumpa support msanii huyo na sio kumponda, na pia promoter huyo aliongeza kwa kusema kuwa kweli ameshajua ana maadui wengi baada ya kutupiwa lawama na wananchi wa kenya kutokana na mkasa huo, lakini amesema yeye na Cannibal hawajavunjika moyo na wataeendelea na kazi kama kawaida.

No comments: