Wednesday, November 20, 2013

MBUNGE WA KAWE AMWAGIA SIFA MSANII DIAMOND

Mbunge Wa Kawe “Kwa Wajanja” Ammwagia Sifa Msanii Diamond Platinumz Kwa Kazi Zake …
Mbunge wa kuchaguliwa jimbo la Kawe “Kwa Wajanja” katika bunge la Tanzania kupitia chama pinzani cha CHADEMA Halima James Mdee, leo amemmwagia sifa msanii mahiri wa Bongo Flava nchini Tanzania, Diamond Platinumz kutokana na uwezo anaouonyesha katika sanaa ya muziki nchini Tanzania.
Kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter mheshimiwa Halima James Mdee amepost tweet za kumsifia Diamond kwa kusema, “Huyu dogo DIAMOND…..Mungu ambariki….ni mtoto wa kitaa…aliyeonyesha kwamba inawezekana..ktk sanaa yetu , kutoka 0-100%. BE BLESSED!”

1 comment:

Anonymous said...

Vijimambo acha uchokozi, kama Halima anasuuzika roho yake na huyo msanii.poa.tuletee habari ingine. Mi namzimia Halima.kamwambie usiku naota kailetea kawe.maendeleo makubwa.