Kiongozi wa Bendi ya Mashujaa Musica, Charles Gabriel ‘Chaz Baba’ na kumsababishia majeraha sehemu mbalimbali za mwili wake.
Chaz Baba akiuguza majeraha aliyoyapata.
Paparazi wetu alifunga safari hadi nyumbani kwake Mwananyamala, Dar kumjulia hali ambapo alisema tukio hilo lilitokea katikati ya wiki iliyopita, Ubungo baada ya kugongwa na gari kwa nyuma.
“Nilikuwa natokea Kimara, nikiendesha pikipiki yangu.
Si unajua tena ile barabara ipo kwenye matengenezo kwa hiyo vizuizi nivingi njiani. Ghafla nilishangaa pikipiki ikigongwa kwa nyuma, nikaanguka.
“Namshukuru Mungu maana mazingira niliyopata ajali ni mabaya sana isitoshe unajua pindi upatapo ajali kuna wengine wanakuja kukusaidia na wengine ni wezi lakini sikuibiwa kitu.
“Nimeumia mkono, kiuno, mguu mmoja wa kushoto na maumivu kwa ndani lakini hakuna sehemu niliyovunjika,” alisema Chaz Baba.
No comments:
Post a Comment