Thursday, November 21, 2013

HAPO ZAMAMI ILIKUWA KAMA HIVI LAKINI SIKU HIVI NI MAMBO YA PAH

Inakuwa nini wanyama wangu? Ama nini? Mishemishe zinakwendaje wanangu wa hapo kitaa cha Moro? Kipande hii barida! Mbona siwasomi wanangu au ndo mmeamua kunimwaga? Basi sawa!
Bila kumbwela, tudei tuzame kwenye stori la chaliiangu Tolu. Yupo tauni Dar kitambo! Chuma kimevuta mtoto mzuri ndani juzikati na vichwa vikapiga mpunga kinomanoma. Lilikuwa pati la kimyakimya bati la kiutu uzima.
Bifoo hajaoa mwana alikuwa anainjoi laifu la kibachela ileile. Alikuwa smati. Mizinguo na stresi zimeanza baada ya kuwa na kifaa insaidi. Yaani ni fulu joto hasira na mawe hakuna!
Mwanangu anakuteli kuwa nawu deizi hata akithinki kutimba mahomu kwa waifu, stimu zinamuishia kozi anajua sheshe la mtoto mkareee atakalokutana nalo. Sam taimu mameni wanachukua wachumba kwa kutazama uzuri na siyo tabia. Hiyo ndiyo shida! 
Truli, Tolu amejikuta akiwa kwenye hadi taimu vibaya mno. Jamaa ana stori f’lani hivi dizaini kama linasikitisha sana. Linagusa mioyo ya wanaume kibwena.

Waifu wa selaa alikuwa maza wa homu tu kwa maana kwamba hana mishe za kutafuta bingo.
Kachaa akaona isiwe kitu, akaamua kumtafutia waifu dili ili ajiajiri aloni.
Akamtafutia mradi wa kuku wa mayai nini na nini! Akampa msingi wa mkwanja wa maana.

Sapraizi ni kwamba huyu waifu wa mshikaji siyo mstaarabu. Hana nidhamu kwa maana ya tabia na hata nidhamu ya mshiko. Ili kufanikiwa kila kitu kinahitaji nidhamu! Yaani hajatuliatulia…huyu mtoto mapepe! Ni mtu wa matumizi sana so haikuchukua taimu ule mradi wa kuku ukafeli kisha akawa anachili tu maskani kwa kumtegemea mwanangu anayepiga dili za kuungaunga tauni.
Akawa mtu wa majungu, kumfuatilia kwa sana msela na kugombana na ndugu, jamaa, marafiki hata majirani wa mshikaji.

Kuhusu ishu za matumizi pale homu, waifu akawa anampeleka jamaa puta kinoma kwani anakompleini kuwa hiyo twenti anayoacha kwa siku haitoshi.

Jambo lingine baya kinoma ni kwamba selaa akiacha foni kwa matebo masti waifu aikague kwa kuperuzi sms na kuchukua foni namba za watu na kuanza kuwaendea hewani kisha kuwapiga mkwara wakae mbali na hazibendi wake. 
Jamaa anajisemea kimoyomoyo kwamba kufanya hivyo yaani kukagua foni yake siyo ishu kiivo kwa maana ya wivu bati ukipitiliza ni majanga.

Kifupi ni mtu ambaye hachelewi kuanzisha varangati na watu wakala nondo za uso.
Kuhusu mambo ya oni bedi ndo kabisa fulu mizinguo. Yaani njiwa wako mwenyewe theni unaanza kumlenga kwa manati! Huo si ni umbulula jamani?

Kuna deizi kifaru wangu akijaa homu akiwa hepi, anakutana na visanga vya waifu kapigana na waifu wa mshikaji wake kisa alikula masanga wakati wa jua kali theni zikampeleka puta! Chezea viroba na jua? Weka mbali na watoto aisee chaliiangu arifu.
Tayari jamaa ameshakwenda kwa maparenti wa saidi zote kukompleini bati anaambiwa kitu cha mereji hakivunjiki so mwana yuu hoi utadhani kabebeshwa gunia la misumari kichwani. Kudadeki!

Chezea mereji weye? Wakati wewe ukimaindi kuingia kuna wana wanaomba kujitoa. Kwa mujibu wa kachaa wangu, huyo waifu wake anaonekana wenge kama vipi akubali kutema mate watu wamchape viboko vya kutosha atakaa sawa tu. Au unaonaje wewe mwana?
Sii yuu neksti wiki. Kwa komenti, tuchekiane kwenye foni hapo juu!

No comments: