Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria, Bwana Fanuel Mbonde akiongea katika kikao chake na viongozi wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora hii leo wakati wa ziara yake fupi katika taasisi hiyo iliyopo mtaa wa Luthuli jijini Dar es Salaam. Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Tume, Mhe. Jaji Kiongozi (mstaafu), Amiri Ramadhani Manento na Katibu Mtendaji wa Tume, Bibi Mary Massay. Lengo la ziara hiyo fupi lilikuwa kufahamiana, kubadilishana mawazo na kukumbushana mambo muhimu.
Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Bibi Mary Massay akijibu baadhi ya hoja zilizotolewa na Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria wakati wa kikao chake na viongozi wa Tume mapema leo.
Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Mhe. Bernadetta Gambishi akichangia hoja wakati wa kikao cha Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria, Bwana Fanuel Mbonde na viongozi wa Tume leo.
Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria, Bwana Fanuel Mbonde akiongea katika kikao chake na viongozi wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora hii leo wakati wa ziara yake fupi katika taasisi hiyo iliyopo mtaa wa Luthuli jijini Dar es Salaam. Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Tume, Mhe. Jaji Kiongozi (mstaafu), Amiri Ramadhani Manento na Katibu Mtendaji wa Tume, Bibi Mary Massay. Lengo la ziara hiyo fupi lilikuwa kufahamiana, kubadilishana mawazo na kukumbushana mambo muhimu.
No comments:
Post a Comment