Advertisements

Wednesday, November 27, 2013

KINA KAKA WAPENI RAHA WAPENZI WENU SI KARAHA

JAMANI hamjambo? Kama ada tumekutana kwenye kona yangu Naa miye, nina imani msemaji ni mmoja siku zote, mshereheshaji akizungumza wote mnakuwa wasikilizaji mpaka atakapotoa ruhusa. Hapo ndipo nilipokuwa napataka, baada ya kuwa kimya sasa nisikilizeni nataka kuzungumza nini.

Leo sitakuwa mzungumzaji bali kumkaribisha mzee mwenzangu Babu Poa, ambaye mlimmisi muda mrefu. Mzee mwenzangu alikuwa katika honeymoon, mwenzenu na utu uzima wake kaongeza mke wa nne, safari hii kaoa mtoto mbichiii utamwambia nini?

Nina imani amerudi na mambo mapya hasa baada ya kusoma mada yangu ya wiki jana niliyozungumzia kumpa mgonjwa dozi kamili na wala usizidishe kwa vile inaweza kuwa sumu itakayomdhuru.
Baada ya kuisoma mada yangu ya wiki jana, naye aliomba wiki hii akandamizie juu yake ili kuwapa wanaume elimu bure. Sikutaka kuwa mzungumzaji saana bali kumkaribisha mwenyewe, Babu Poa karibu.

“Asante Bi Nasra, sitaki kuzunguka sana bali kwenda kwenye kusudio la mimi kuwa hapa. Jamani leo nataka kugandamizia juu ya mada ya wiki jana, nina imani kila mmoja aliisoma na kuona jinsi wanaume wengi tunavyotumia nguvu nyingi katika tendo la ndoa bila akili na kulifanya kuwa mateso badala ya starehe.
Siku zote mapenzi ni raha na mkimaliza mpeane asante na mabusu, siyo mwenzio kageukia ukutani huku kakunja uso na ugonjwa wa tumbo juu.

Wewe ukinyanyuka unajiona mwanaume kwa kumuumiza mwenzio hata, ukitaka tena hawezi kwa vile tayari ushamtia ugonjwa. Hebu tegeni sikio ili tuligeuze tendo la ndoa burudani na si mateso. Leo nimeona kuna umuhimu wa kuwarudisha wanaume darasani ili tufanye wapenzi wetu wafurahie safari na mkifika mwisho kila mtu atue mzigo wake salama huku mkishangilia kwa raha ya safari.

Jamani sote tunajua huwezi kuingia shambani na kuanza kulima bila kufanya maandalizi. Vivyo hivyo katika mapenzi. Hakika kabla ya kumuingilia mwenzio muandae kwa kuzigusa sehemu zenye kuleta msisimko ambazo hufanya akili na mwili kujiandaa kwa kufungua njia huku ukitengeneza ute ili mkikutana msiumizane wala kuchubuana.

Kama huzijui, mshike taratibu kwenye nyayo, chuchu kwenye pachipachi zote kichwani kunyonya ndimi taratibu. Sehemu hizi ukizigusa taratibu humtengeneza mwanamke na kuwa tayari kwa tendo.
Nini kinatakiwa kufuatwa baada ya hatua ya awali kutekelezwa kwa umakini? Si kingine ni tendo lenyewe. Sehemu hii wengi tunaikosea kwa kutumia nguvu nyingi bila kujua urefu wa kina cha maji tunaingiza mguu.

Sehemu hii inataka akili nyingi na ufundi kuliko nguvu kwa vile unayefanya naye mapenzi ni mwanadamu siyo gogo hivyo inatakiwa kutumia akili nyingi na nguvu kidogo. Hata katika mitindo ya mapenzi wakati wa tendo lazima tuyajue maumbile ya wenzetu kuliko kuwaumiza bila kujua.
Usimpinde mwenzio wakati ukijua maumbile yake mafupi na yako marefu, kwa kufanya hivyo lazima utamletea matatizo ya tumbo hata kumsababishia kushindwa kuzaa.

Tunatakiwa tutumie mitindo yenye kuleta raha na si maumivu kama ilivyoelezwa na Anti Nasra wiki jana. Tukifanya hivyo lazima wapenzi wetu watafurahia na kutamani tena na si kulichukia tendo hilo.
Kwa leo yangu yanatosha niwarudisheni kwa Anti Nasra amalizie.”
Asante Babu Poa nina imani kila kitu umekiweka wazi, jamani wanaume tupeni raha si karaha yangu kwa leo ni hayo tukutane wiki ijayo.
Ni mimi Anti Nasra, Shangingi Mstaafu. 

GPL

1 comment:

Anonymous said...

swadaktaaa...message received!hata kama unayo kubwa manjonjo yana umuhimu wake ati! tena siyo matayarisho ya one minute, muandae mwenzio vilivyo