ANGALIA LIVE NEWS

Friday, November 1, 2013

KUBEZWA, KUDHARAULIWA NA KUCHEKWA NI DARAJA LA MAFANIKIO

WIKI iliyopita utakumbuka nilianza kuzungumzia mada yenye kichwa cha habari kilichopo hapo juu. Ni mada iliyoonesha kuwagusa wengi.

Kwa simu na meseji nilizopokea, nimegundua wengi wanashindwa kufanikiwa kwa kukata tamaa kutokana na kuchekwa na kudharauliwa pale wanapoanza safari ya kuelekea kwenye mafanikio.

Kikubwa tutambue kwamba, kuchekwa, kudharauliwa na kubezwa ni daraja la kuelekea kwenye mafanikio hivyo tuchukulie kama changamoto na kutupa hasira za kupambana zaidi.

Aidha, tambua Mungu alikuumba kwa mfano wake, wewe ndiye unayemwakilisha chini ya jua, hakuna litakalokushinda kabisa labda ujiwekee mazingira ya kushindwa. Wanaokucheka ni binadamu tu, Mungu yuko pamoja nawe, hata kama unapita katika wakati ambao kila binadamu anaamini hutashinda, jipe moyo!

Jambo la msingi…

Jambo la msingi hapo ni wewe kumwamini Mungu, kufanya kazi kwa nguvu, bidii, malengo na maarifa ya hali ya juu huku ukiamini kuwa mafanikio ni lazima maishani endapo tu utadhamiria kwa dhati kuyatafuta. Jiamini kuwa wewe ni mtu wa pekee mno katika dunia hii, hakuna aliyeumbwa kufanya unachotaka kukifanya!

Ni wewe tu! Piga hatua, kazana kwa kila jambo, waombee wanaokubeza ili siku moja wakusalimie kwa heshima huku wakikunyenyekea! Hayo yatatimia endapo tu utaamua.

Nilishawahi kuandika huko nyuma kuwa, mafanikio maishani hayaji kwa bahati mbaya kama ajali, mafanikio ni kupanga na kuchukua hatua madhubuti juu ya mipango hiyo. Usiishie kupanga tu, weka mikakati madhubuti ambayo itakuwezesha kufika pale unapopataka.

Jifunze na kujielimisha juu ya hicho kitu na baada ya hapo sasa chukua hatua kwa kudhamiria huku ukiziba masikio juu ya dharau na vicheko vyao! Amini kuwa ni lazima utimize ndoto zako.

Jambo la muhimu ni kujua unachokitaka hapa duniani. Ukijua unachokitaka ni hatua ya kwanza kukipata. Mwandishi mmoja maarufu wa vitabu vya saikolojia duniani, Johan Wolfgang Van Goeth aliwahi kusema; To get what you want, you must first decide what you want, knowing what you want is the first step towards getting it (Kupata unachokitaka, ni lazima kwanza uamue unachokitaka, kujua unachokitaka, ni hatua ya kwanza kuelekea kukipata).

Wewe amua tu unachokitaka maishani halafu chukua hatua kwa kumaanisha, achana kabisa na biashara ya kusikiliza maneno ya kuvunja moyo na dharau za watu, piga magoti umuombe Mungu awajaalie afya njema wanaokudharau na kukucheka kwa sasa, ili ukifanikiwa wayashuhudie matunda hayo!

Narudia tena, kamwe usiwachukie hata kidogo, badala yake dharau zao, vicheko vyao na kukubeza kwao vigeuze kuwa kuni za kuchochea moto wa mafanikio yako.

Ni watu muhimu mno, dharau zao ni madaraja ya mafanikio, ni lazima wawepo watu wa kukudharau na kukucheka ili ufanikiwe. Mungu amewaleta maishani mwako ili kukuimarisha katika mbio zako za kusaka mafanikio maishani. Fanya kazi kwa nguvu na juhudi zote, hakika wewe ni mshindi.

Futa kabisa CD ya neno kushindwa, weka CD ya neno USHINDI! Hakuna kilicho chema ambacho huja kwa njia rahisi maishani ndugu yangu, kupata mafanikio ni lazima utokwe na jasho, lazima uumie, lazima ulie, lazima ukatishwe tamaa.

Ukivumilia yote hayo, mwishowe lazima uwe mzuri. Uliumbwa kuwa mshindi, epuka mambo ambayo hayana faida yoyote maishani, kuwa bize, kuwa ‘serious’, dhamiria kuwa na mafanikio na si kitu kingine kabisa maishani mwako! Usihesabu udhaifu ulionao, hesabu nguvu kuu iliyomo ndani yako.

Nikiwa naelekea mwisho kabisa mwa makala haya, naomba nikuambie neno moja muhimu sana maishani kuwa, hakuna aliyeumbwa akiwa tajiri wala maskini, vyote hivyo ni matokeo ya jinsi tunavyowaza na kutenda mambo maishani! Wewe ni mtu mkubwa mno, maishani ni uchaguzi, kwenda kulia au kushoto unachagua mwenyewe, kusuka au kunyoa uchaguzi ni wako. credit GP

No comments: