
KUONGEZEKA kwa pilikapilika za maisha na maendeleo ya sayansi na teknolojia, vimesababisha matatizo kwa wanandoa kuzidi kuongezeka kila kukicha.
Kupoteza hamu ya tendo kwa wanawake na wanaume, ni miongoni mwa matatizo ambayo yanawasumbua wanandoa wengi kiasi cha kufikia hatua ya kuhisi kuna usaliti unaendelea. Leo tutalizungumzia tatizo hili kwa kina kuanzia jinsi linavyotokea na namna ya kulishughulikia.
CHANZO CHA TATIZO
Chanzo cha tatizo la kukosa hamu ya kufanya tendo, kimegawanyika katika makundi mawili; matatizo ya kimwili na matatizo ya kisaikolojia.
MATATIZO YA KIMWILI
Ugonjwa wa Anaemia (upungufu wa seli nyekundu za damu) unatajwa kuwa chanzo kikuu cha tatizo hili kwa sababu huambatana na upungufu wa madini ya chuma (iron) ambayo hufanya kazi ya kuusisimua mwili na kuongeza hamu ya tendo.
Wanawake wanapokuwa hedhi, hupoteza kiwango kikubwa cha madini haya ambayo hutolewa mwilini kupitia damu ya hedhi, hivyo kuchangia kwa kiasi kikubwa kupoteza hamu ya tendo.
Ugonjwa wa kisukari nao unatajwa kuchangia kwa kiasi kikubwa kupoteza hamu ya tendo.
Ulevi na matumizi ya madawa ya kulevya ni sababu nyingine inayochangia tatizo hili. Mwanamke anayekunywa kiwango kikubwa cha pombe au anayetumia madawa ya kulevya, hupoteza kabisa hamu ya tendo na sehemu zake za siri huwa kavu.
Itaendelea wiki ijayo. GPL
No comments:
Post a Comment