MAHAKAMA kuu kanda ya Mbeya, imemwachia huru mtuhumiwa aliyekuwa amehukumiwa kifungo cha maisha na viboko 10 na kutumikia kifungo hicho tangu mwaka 1999 kwa kosa la ubakaji baada ya kukata rufani.
Hukumu ya rufaa hiyo imetolewa na Jaji wa Mahakama kuu kanda ya Mbeya, Samweli Karua, baada ya rufaa iliyowasilishwa mahakamani hapo namba 17 ya mwaka 2013, ambapo mtuhumiwa Isack Righton(34) ameachiwa huru kutokana na vegozi vya hukumu dhidi yake kukiuka baadhi ya vifungu.
Awali akisoma maelezo ya kosa la Mtuhumiwa huyo, Mwendesha mashtaka wa Serikali, Ahmed Sitambuli alisema mtuhumiwa huyo alifikishwa mbele ya mahakama ya Wilaya ya Mbozi Juni 1, 1999 akituhumiwa kutenda kosa la ubakaji kinyume na kifungu cha 130 na 131 (3) sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.
Alisema mtuhumiwa huyo alidaiwa kutenda kosa hilo April 4, 1999 wakati huo akiwa na miaka 20 baada ya mhanga wa tukio hilo(jina limehifadhiwa) ambaye alikuwa anaishi na wazazi wake wakiwa wapangaji katika nyumba iliyokuwa ikimilikiwa na mtuhumiwa huyo.
Ilidaiwa kuwa siku ya tukio lililofanyika katika kijiji cha Kaloleni Tnduma wilayani Momba majira ya saa moja jioni, wazazi wa Mhanga walikuwa wamemwacha binti yao nyumbani ili hali wao wakiwa shambani ambapo baada ya kurudi walimsikia binti yao akilia huku akitokea chumbani kwa mtuhumiwa na kumkuta akiwa na damu pamoja na mbegu za kiume sehemu zake siri baada ya kufanyiwa uchunguzi.
Hata hivyo katika hukumu ya Jaji Karua katika rufaa ya mtuhumiwa huyo, amesema hukumu iliyokuwa imetolewa na Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Mbozi, FCP Mdendemi ilikuwa na makosa ya kiushahidi.
Alisema hukumu hiyo ilikuwa na makosa matatu ambayo aliyataja kuwa ni uwasilishaji wa kielelezo ambacho ni Fomu namba tatu ya Polisi(Pf3) kuwasilishwa mbele ya mahakama na shahidi ambaye ni mzazi wa mhanga Moses Simwanza badala ya Daktari aliyemfanyia uchunguzi.
Aliitaja sababu ya pili kuwa ni pamoja na binti aliyefanyiwa kitendo hicho kushindwa kufika mahakamani kutoa ushahidi jambo ambalo ni kinyume na utaratibu wa ushahidi huku sababu ya tatu ikiwa ni ushahidi uliotolewa mahamani hapo kuwa haukutosheleza kumtia hatiani mtuhumiwa kwa sababu ya kutolewa na mashahidi watatu ambao ni baba mzazi wa mhanga, mama mzazi na Askari Polisi Wp 381 Sajent Neema.
Kutokana na maelezo hayo Jaji karua amemwachia huru mshtakiwa huyo ingawa amesota gerezaji kwa miaka 14 tangu kuhukumiwa, ingawa mtuhumiwa huyo katika maelezo yake alikana kuhusika na tukio hilo na kwamba hakuwepo eneo la tukio.
Na Mbeya yetu
No comments:
Post a Comment