8. HUCHEZI KWA DAKIKA ZA KUTOSHA
Nukuu kutoka kipengele kilichopita “Humpi mpaka akatosheka”, kwamba unaweza kupiga mbizi kwa muda mfupi na akawa ametosheka ikiwa tu utatumia muda wako wa kutosha wakati wa jeramba, inaweza ikakufanya uchanganyikiwe kama tu hutasoma kwa mtindo wa katikati ya mstari (between the line).
Muda mfupi ambao nimeueleza hautakiwi kuwa chini ya dakika 15. Yaani jeramba umempa la kutosha mpaka ameelekea, amelendemka, hapo sasa unatakiwa ujipe angalau muda huo kwa kupiga mbizi ndipo ukamilishe mzunguko wa kwanza. Ukifanya hivyo, hakuna atakayekulaumu kwamba huna ubavu.
Kama ubavu unao, unaweza kuendelea kuogelea kwa muda unaoweza lakini ni vizuri ukawa unawasiliana na mwenzi wako, kwani unaweza kudhani sifa kutuama kwa dakika nyingi lakini kumbe ukawa unamboa mwenzako, tena zaidi ukawa unamuumiza.
Kadhalika, siyo kwamba hizo dakika 15 zinatosha kihivyo, hapana. Ila kitaalamu inashauriwa angalau ujibane ufikishe muda huo, kwani hapo ndipo utafanikiwa kumfikisha mwenzi wako kileleni. Bila shaka hilo ndilo hitaji lako, kwa hiyo simama imara ufikishe dakika hizo.
Itambulike kwamba hili ni kosa ambalo linajulikana vizuri sana, yaani ni rahisi mno kulibaini inapokuja mada yoyote inayohusu makosa ya wanaume faragha. Tatizo kubwa hapa ni wanaume kukosa utulivu kwa kulivamia tendo kwa pupa, ndiyo maana hukosa uwezo wa kujidhibiti.
Hata hivyo, inaeleweka pia ni ndoto ya kila mwanaume kupiga mbizi kwa muda mrefu ili amtosheleze mwenzi wake, kadhalika aonekane kidume wa ukweli. Tatizo hapa ni kwamba wengi hawajui ni muda gani watumie, matokeo yake wanachezacheza kisha wanatangulia kileleni kabla ya wakati.
Mtaalamu wa masuala ya mapenzi, Julie Orlov, anasema katika makala yake ya mapenzi kuhusu faragha, yenye kichwa “Most Dangerous Mistakes of Men In Bed”, anasema kuwa wanaume huchukulia suala la muda wa kupiga mbizi kwa muda mrefu ni gumu wakati siyo kweli.
Anasema: “Kama mwanamke najua, nikiwa pia mtaalamu na mtafiti wa masuala ya uhusiano, hili halipingiki kwamba wanawake hatupendi kukatishwa kufika kileleni. Tunachukizwa sana na wanaume ambao muda wao wa tendo ni chini ya dakika 10.”
Anaendelea: “Nilipoamua kusoma kuhusu faragha, nilizungumza na wanawake zaidi ya 200, jawabu nililopata ni kuwa mwanaume anatakiwa kumfanyia mwanamke wake maandalizi ya kutosha na baada ya hapo atumie angalau dakika 15 kupiga mbizi ndipo mambo huwa murua.
“Muongozo kwa kila mwanaume hapa ni kutuliza akili, ajiamini na amuone mwanamke aliyenaye ni wake na huduma anayompa inamsafirisha katika ulimwengu unaotakiwa, hapo atafanikiwa. Wanawake pia wanapaswa kuwajenga wanaume wao kisaikolojia na kuwapa sapoti ili wapige mbizi kwa dakika zinazofaa.”
9. KUTOTAMBUA VITABIA VYA MWENZI WAKO
Kwa faida yako ni kwamba wanawake huwa na vitabia vya ajabuajabu hasa linapokuja suala la faragha. Kosa hapa ni kwa wanaume kutotambua kwamba hivyo ni vijimambo, badala yake kuamua kuhukumu kwa imani kwamba hizo ni tabia halisi za mwanamke husika.
Inaweza kutokea mwanamke akawa na tabia ya kuwa mgumu kuelekea kwenye safari mnayotaka kwenda. Si kwamba hataki, la hasha! Anahitaji kabisa lakini kukubali haraka au kujiachia anaona ataonekana maharage ya Mbeya, kwa hiyo anaamua kubana kwanza.
Sikufichi, atakapojifanya anabana, nawe ukaamua iwe hivyo, utamuumiza kupita kiasi.
Itaendelea wiki ijayo.
GPL
No comments:
Post a Comment