Kutoka kushoto ni mdhamini, Ali Sungura, Balozi wetu Uingereza , Mheshimiwa Peter Kallaghe, Malkia Kassu, sahiba mkuu Aisha Mohammed na Afisa Balozi, Allen Kuzilwa.
Picha na Said Surur
Jumuiya ya Madola ilianzishwa karne ya 19 kushirikisha mataifa chini ya Uingereza. Mwaka 1949 chini ya himaya ya kifalme ma nchi huru zilihusishwa. Toka 1973 mikutano ya wanajumuiya imefanywa kila baada ya miaka miwili chini ya Malkia Elisabeth. Lakini Jumuiya ya Madola si tu siasa na mikutano. Ina mirengo mbalimbali ikiwemo michezo, uchumi, utamaduni , familia, urembo wa mavazi, sura, fikra na tabia.
Mashindano ya kuwatafuta warembo wa kike na wa kiume hufanywa kila mwaka. Taji zinazoshindaniwa ni Mrembo wa Vijana wa Jumuiya ya Madola, Mrembo wa Jumuiya ya Madola ya Kimataifa na Mrembo wa Kimataifa wa Jumuiya hiyo. Malengo ya mashindano haya ni mengi na baadhi ni...
• Kuendeleza maisha ya wananchi duniani
• Kuondoa umaskini, hasa ule unaowahusu watoto na mama zao, familia, michezo, maisha na afya ya wanyama
• Kampeni za maonyesho ya kusaidia maendeleo ya kijumuiya
• Kuendeleza mashirika ya fadhila
Na kadhalika.
Mtanzania, Malkia Kassu ( wa tano toka kushoto) akiwa na washindi wenzake - wote wamevalia taji na kubeba vikombe vya ushindi.
Picha na Jay Pedram
Mashindano ya 2013 yalikuwa mjini London, Jumamosi Novemba 16 na kwa mara ya kwanza yalikuwa na mshiriki toka Tanzania. Malkia Kassu ( jina la kuzaliwa Mulki Kassu Miraj) alichaguliwa malkia wa Tanzania na bara zima la Afrika. Wateuzi wa ushindi huo hawakuangalia tu sura, bali tabia, fikra, hamasa na msimamo wa kimaendeleo wa mhusika. Washindani walitoka mataifa mbalimbali duniani.
Malkia Kassu aliyezaliwa Tanzania 1991 akahamia Ulaya na familia (akiwa na umri wa miaka minne) amepata mafanikio haya kwa kujituma mwenyewe. Hakuna chombo chochote cha serikali kilichomsaidia. Alinieleza kabla ya kupata ushindi:
“Ninataka kuiwakilisha nchi yangu na kuwasaidia wenye maisha magumu, niifanye dunia iwe mahali pazuri zaidi. N’nafahamu si kazi rahisi; ila nina hakika kila mmoja wetu akijumuika na mwenzake mabadiliko mema zaidi yatafanyika. Tanzania ni nchi ya amani na ninaamini amani na mapenzi vyaweza kuongezeka katika jumuiya zetu.”
Malkia Kassu- na taji lake- akipongezwa na marafiki, Andrew Matt na Aisha Mohammed.
Picha na Jay Pedram
Kinyume na vijana wanaozaliwa au kukulia Uzunguni wakashindwa kuongea Kiswahili , Malkia Kassu anazungumza Kiswahili fasaha kutokana na wazazi wake kumkazania asisahau atokako. Akiwa mdogo alihudhuria madarasa ya lugha ya Kiswahili. Mbali na Kiswahili anazungumza pia Kiswidi, Kiingereza fasaha “na Kiarabu na Kisomali cha kubabaisha.”
Anasema ari yake kuendeleza na kuondoa umaskini Tanzania (na bara Afrika) ilianza kupamba moto aliporudi likizo mwaka jana.
“Kila tukisimama na gari katika taa nyekundu n’liwaona watoto wadogo wakiomba omba; wengine wametumwa na wazazi wao. Ilinigusa sana, maana kila mtu duniani anatakiwa awe na ndoto. Hawa watoto ni kama wamezimishwa ndoto – hawana la maana maishani. Niliumia pia kuona walemavu wengi wasiohudumiwa kabisa.”
Aliamua lazima afanye bidii kuchangia kuondoa janga hili badala ya kulaumu tu serikali na viongozi.
Karibuni mwanamke huyu mwenye miaka 22 alianzisha kampuni iitwayo “Strawberry and Champagne” yenye azma ya kubadili maisha ya watu na jamii kupitia starehe na sanaa za maonyesho. Sasa hivi anafanya kazi hoteli ya Spoons, mjini London, huku akitafuta wasanii na vipaji vipya.
Taji la ushindi wa Miss Commonwealth Africa limeyaweka matazamio yake katika safari njema.
Atakuwa na uwezo zaidi wa kukutana na viongozi na mashirika mbalimbali ya Jumuiya ya Madola na hatimaye kutimiza ndoto ya kuchangia kuleta maendeleo Tanzania na Afrika.
Tumpigie makofi na kumwombea Mungu amsaidie. Kwani juhudi na furaha za mpiganaji huyu ni zetu wote.
Kila la kheri, Malkia wetu!
Kinyume na vijana wengi wanaozaliwa au kukulia Uzunguni , Malkia Kassu anazungumza Kiswahili fasaha kutokana na wazazi wake kumkazania asisahau atokako. Akiwa mdogo alihudhuria madarasa ya lugha ya Kiswahili. Mbali na Kiswahili anazungumza Kiswidi, Kiingereza fasaha “na Kiarabu na Kisomali cha kubabaisha.”
Anasema ari yake kuendeleza na kuondoa umaskini Tanzania (na bara Afrika) ilianza kupamba moto aliporudi likizo mwaka jana.
“Kila tuliposimama na gari katika taa nyekundu n’liwaona watoto wadogo wakiomba omba; wengine wametumwa na wazazi wao. Ilinigusa sana, maana kila mtu duniani anatakiwa awe na ndoto. Hawa watoto ni kama wamezimishwa ndoto – hawana la maana maishani. Niliumia pia kuona walemavu wengi wasiohudumiwa kabisa.”
Aliamua lazima afanye bidii kuchangia kuondoa janga hili badala ya kulaumu tu serikali na viongozi.
Malkia Kassu akiwa na mwanamuziki maarufu Diamond...
Karibuni mwanamke huyu mwenye miaka 22 alianzisha kampuni iitwayo “Strawberry and Champagne” yenye azma ya kubadili maisha ya watu na jamii kupitia starehe na sanaa za maonyesho. Sasa hivi anafanya kazi hoteli ya Spoons, mjini London, huku akitafuta wasanii na vipaji vipya.
Taji la ushindi wa Miss Commonwealth Africa limeyaweka matazamio yake katika safari njema.
Atakuwa na uwezo zaidi wa kukutana na viongozi na mashirika mbalimbali ya Jumuiya ya Madola na hatimaye kutimiza ndoto ya kuchangia kuleta maendeleo Tanzania na Afrika.
Tumpigie makofi na kumwombea Mungu amsaidie. Kwani juhudi na furaha za mpiganaji huyu ni zetu wote.
Kila la kheri, Malkia wetu!
-London, Jumatano, 27 Novemba, 2013
www.freddymacha.com
No comments:
Post a Comment