
Kutoka kushoto ni wanenguaji Aisha Madinda, Otilia Boniface na Marehemu Mwantum Athuman wakilishambulia jukwaa.
Mnenguaji wa Bendi ya Extra Bongo, Mwantum Athuman amefariki dunia jana katika Hospitali ya Mwananyamala, jijini Dar es Salaam baada ya kusumbuliwa na ugonjwa wa mapafu kujaa maji. Marehemu Mwantum atazikwa leo saa 10 katika Makaburi ya Mburahati, Dar. Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. AMEN!-GPL
No comments:
Post a Comment