Advertisements

Tuesday, November 19, 2013

MBWA WA MCHUNGAJI ANYONYESHA WATOTO WA NGURUWE

Mbwa anayenyonyesha watoto wa Nguruwe Iringa 
Mchungaji Daniel Kisonga akimwonyesha mbwa anayenyonyesha watoto wa Nguruwe
Mbwa huyo akinyonyesha watoto wa Nguruwe huku mtoto wake (kulia) akishindwa kunyonya 
Huyu ndie Mbwa anayenyonyesha watoto wa Nguruwe Iringa 
Katika hali isiyo ya kawaida kuzoeleka ni baada ya wakazi wa Ilala katika Manispaa ya Iringa leo kushuhudia maajabu ya dunia baada ya kushuhudia tukio la aina yake kwa mbwa kuwachukua watoto wa nguruwe na kuwalea kwa kuwanyonyesha maziwa yake.
Tukio hilo limetrokea machi 15 mwaka huu majira ya asubuhi baada ya nguruwe wa mmoja kati ya watumishi wa mungu (mchungaji ) Daniel Kisonga kushuhudia mbwa huyo ambae alikuwa amezaa watoto watatu na kufariki wawili na kubakia na mtoto mmoja na hivyo kulazimika kuingia katika banda la nguruwe na kubeba watoto wanne wa nguruwe na kuamua kuwalea na kuwapa huduma zote ikiwemo ya kuwanyonyesha kwa upendo watoto hao wa Nguruwe bila kuwadhuru.
Akizunguza na mwandishi wa habari hizi leo mchangaji Kisonga amesema kuwa ni vigumu kuamini kuna mbwa akinyonyesha watoto wa nguruwe wakati kwa kawaida mbwa amekuwa ni mnyama hatari kwa nguruwe hao hasa pale wanapozaliwa .
Amesema kuwa mbwawa wamekuwa wakiingia katika mazizi ya nguruwe na kuwala nguruwe hao baada ya kuzaliwa ili imekuwa tofauti kwa mbwa baada ya kuamua kulea watoto wa nguruwe .

Hata hivyo amesema yawezekana ni maajabu ya dunia ila pia yawezekana ni dalili za siku ya mwisho kama ambavyo zimepatwa kutabiliwa katika maandiko matakatifu kuwa siku za mwisho yatajitokeza mambo mengi ya ajabu ambayo binadamu ni vigumu kuamini mambo hayo.

Japo upande wa wadau mbali mbali wamehoji nguruwe hao iwapo wataendelea kunyonya maziwa na mbwa wataliwa na binadamu ama lah ! kutokana na nyama ya mbwa kwa kawaida kutoliwa na binadamu sasa iweje kwa nguruwe hao kunyonya maziwa ya mbwa

3 comments:

Anonymous said...

Iringa! Nguruwe kitowe na mbwa nyama tamu na ugali,

Anonymous said...

kula nguruwe ni sawa na kula mbwa

Anonymous said...

In Iringa, both of those animal species are interchangeably used for barbecue which traditionally come with three sides; ugali, steamed marijuana leaves, and ulanzi.