Thursday, November 21, 2013

MHE. BALOZI LIBERATA MULAMULA AMTEMBELEA BALOZI EDUARDO MEDINA ICAZA WA MEXICO WASHINGTON DC

Mhe. Balozi Liberata Mulamula katika mazungungumzo na Mhe. Balozi Eduardo Medina-Mora Icaza Ofisini kwa Balozi huyo Washington DC pamoja na taswira mbali akiwa na Balozi huyo.
Mhe. Liberata Mulamula, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani na Mexico jana alimtembelea Mhe. Eduardo Medina-Mora Icaza, Balozi wa Mexico nchini Marekani. Balozi Mulamula alimtembelea Balozi Eduardo ili kujitambulisha na kufahamiana nae. Katika mazungumzo yao,Balozi Mulamula alimweleza Balozi huyo wa Mexico historia ya uhusiano wa Tanzania na Mexico tangu Enzi ya Mwalimu Julius Nyerere kupitia Taasisi ya South South Commission. Aidha, alimkumbusha uhusiano wa karibu na wa siku nyingi baina ya chama cha Kimapinduzi cha Mexico(PRI) na Chama cha Mapinduzi (CCM) cha Tanzania ambapo wakati wa kuapishwa Rais mpya wa Mexico Mhe. Enrique Nieto mwezi Desemba 2012, Mhe. Dr. Mohamed Gharib Bilal, Makamu wa Rais alimwakilisha Mhe.Rais Jakaya Kikwete,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika hafla hiyo. Sambamba, Mhe. Balozi Mulamula alipata wasaa pia wa kupata taarifa za muda ambao atawasilisha Hati zake za Utambulisho kwa Rais wa nchi hiyo mapema mwakani.

No comments: