Mh.Mwigulu
Nchemba akiwa na uso wa Furaha mara baada ya kuwasili kwenye Mkutano
wa Hadhara kijiji cha Kibaya kata ya Ndago mapema hii leo
Tar.11/11/2013 |
Mh.Mwigulu Nchemba akichangia papo kwa papo ujenzi wa Kituo cha Afya
kijiji cha Kibaya,Ujenzi ambao unaendelea kwa jitihada za wananchi na
huyu Mbunge wao.Pichani ni Mtendaji wa kijiji akitoa neno la shukrani
kwa Mh.Mbunge kwa namna alivyokuwa nao bega kwa bega kuanzia kwenye
miradi ya maji na barabara,shule na Umeme na sasa kwenye ujenzi wa
Kituo cha Afya kijijini hapo ndani ya kata ya Ndago
Pichani ni Umati wa wananchiwa kijiji cha Songa Mbele wakimpokea kwa
shangwe Mbunge wao Mh.Mwigulu Nchemba hii leo kwenye Mkutano wa hadhara
kwaajili ya kuzungumzia maendeleo ya kata ya Ndago na jimbo la Iramba.
Ni shauku kubwa kwa Wanafunzi kukutana na Mbunge wao,Pichani ni
Mh.Mwigulu Nchemba akisalimina na Wanafunzi waliokuwa wakitokea shule
na kukutana nao njiani wakati wa ziara yake ya kuzungukia miradi ya
maendeleo kata ya Ndago hii leo.
Picha ni mapokezi ya Mh.Mwigulu Nchemba kijiji cha Lunzinzi kata ya Ndago wakati wa mkutano wa hadhara hii leo.
Mh.Mwigulu Nchemba na Naibu katibu Mkuu wa CCM Tanzania bara
akizungumza na wananchi wake kuhsu hatua mbalimbali za miradi ya
Maendeleo hususani Umeme,Afya,Maji na Barabara inayoendelea kujengwa
ndani ya kata ya Ndago.Ambapo katika mrejesho wake kwa Wananchi
amewaeleza kuwa Umeme umeshaanza kuwaka kwenye vijiji mbalimbali na
kwenye kijiji hiki nguzo zimeshawekwa na mapema mwaka ujao umeme
utawaka.Pia kuhusu maji visima vimeshaanza kuchimbwa na Ndago mjini
maji yameshaanza kutoka na kusaidia wananchi wote wanaozunguka Ndago
Mjini.
Viongozi wa serikali na chama cha Mapinduzi wakiongozana na Mbunge wao
walipata nafasi ya kutembelea moja ya eneo linaloandaliwa kwaajili ya
Bwawa la maji ndani ya kijiji cha Songa Mbele kata ya Ndago.Mbunge
amewahakikishia kuwa atatoa mchango wake wa hali na mali kuhakikisha
Bwawa hilo linakamilika kabla msimu wa Mvua haujaanza mwishoni mwa mwaka
huu.
Na Ibrahim Makunda.
Mpango wa kusambaza umeme huo umeshaanza na baadhi ya vijiji umeshaanza kuwaka, Pia Mbunge huyo amezungumza na wananchi wa kata ya Ndago kuhusu barabara ambayo imekamilika na inapitika kiurahisi kutoka Ndago kwenda singida Mjini,lakini pia ametoa mrejesho wa Ujenzi wa vituo vya Afya kila kijiji cha kata ya Ndago na namna alivyofanikisha kupatikana kwa Magari mawili kwaajili ya Hospitali ya Ndago kwaajili ya kutoa huduma kata nzima na jimboni hapo.
Katika hali ya kuonesha namna Mbunge huyo yupo na Wananchi bega kwa bega amechangia Cash ujenzi wa Vituo kadhaa vya huduma za Afya,Pia amechangia papo kwa papo vikundi vya Uimbaji na vyaasili pamoja na timu za Mipira kwaajili ya kuimarisha umoja miongoni mwa Wananchi wake.
Kwenye sekta ya Elimu Mh.Mwigulu Nchemba amesambaza vitabu vyenye thamani ya Milioni 16 za Kitanzania katika kata nzima ya Ndago,huku akichangia madawati kila shule yenye tatizo la Madawati.
Pamoja na hayo,Mbunge huyo ametoa nafasi kwa Wananchi wake kuuliza maswali ya papo kwa papo na kujibiwa vyema na yeye mwenyewe akishirikiana na viongozi wa serikali aliombatana nao hususani sekta ya kilimo na Ufuatiliaji wa Mapato na Matumizi ya serikali za vijiji.
Pia amewasihi sana wananchi wake kujishughulisha na kazi za kilimo kuhakikisha wanaondokana na njaa,amewataka Wananchi kujiandaa na kilimo msimu huu wa mvua unapoanza,pembejeo zimeshafika wilayani na kila mmoja anahaki ya kupata.Hivyo fursa pekee ya kuondona na njaa na vyakula vya misaada ni kujikita kwenye uzalishaji kupitia kilimo na kaucha kuharibu vyanzo asili hasa ukataji ovyo wa misitu.
Mwisho kabisa Mh.Mwigulu Nchemba aliomba Wananchi wa Ndago kudumisha amani na mshikamano huku akiwambia kuwa Kinachomuunganisha yeye na WanaIramba ni maendeleo tu,mengine yanafuata.Hivyo basi WanaIramba wanapaswa kuhakikisha wanambana pale ambapo hajatimiza,pia kuibana timu yake ya kazi ndani ya jimbo kuhakikisha shughuli zote za maendeleo zinafanyika kwa wakati na kwa ufanisi.
No comments:
Post a Comment