Nina mpenzi wangu ambaye yuko chuo fulani hapa Dar lakini kutokana na maamuzi yetu tuliamua aishi mtaani badala ya Hostel. Huyu msichana nilianza nae mahusiano kwa kipindi kirefu sana na hata tumefikia kuvalishana pete na nyumbani kwao nafahamika pia.
Kutokana na shughuli zangu nyingi kua mikoani hua tunakutana kwa baadhi ya wikiendi tu ninapokuja hapa Dar.
Basi Ijumaa hii nikaona sio vibaya kum-surprise my wife to be. Nikatoka zangu mkoani na shauku ya kujiandaa kwenda kwa P-square na mamaa.
Nilipofika pale Geto kwake hali sikuielewa. Nikaona sio mbaya kubisha hodi. Niligonga kidogo tu sauti yenye hasira na mikwaruzo ikatoka ndani. "Wewe Nani"???
Nikajibu kwa kujiamini nikijua wako discussion na wenzake.. "Mimi ni Edwin"
Ndani nikasikia kama wanabishana kidogo.
Ghafla jamaa akafungua mlango na kuniuliza huku amekasirika wewe nani? Nikajibu kwa kujiamini. "Kama Grace yupo ndani muulize Edwin ni nani?"
Basi Grace alipoulizwa akakana kunifahamu. Hapo jamaa akaanza kunishushia kipigo. Kutokana na mwili mdogo nilionao jamaa alinipga kwa kweli huku akitishia kunipigia kelele za mwizi.
Basi baada ya pale nikaenda hospital kupata matibabu. Nikaamua kumtaarifu mama yake Grace. Mama Grace alishangaa sana na kudai mbona Grace alimtaarifu tumeachana kwa Mwezi sasa?
Nikachanganyikiwa zaidi. Nilipopeleleza zaidi kwa rafiki yake mmoja, nikagundua jamaa ndio anamgharamia Grace kila kitu na kias nilichotoa kwa Grace ilikua hela ya chumvi tu..
Hapa nilipo nina maplasta usoni na sehemu nyingine.
Nisaidieni nichukue hatua Gani kisheria juu ya huyu jamaa? Je akisema nilitaka kuiba nitajitetea vipi? Ushauri wenu ni muhimu sana
Note
Nimetumia majina ya kweli ili kama Grace yupo humu ndani ujumbe umfikie na ajue ameniumiza sana moyoni kwa usaliti aliouonyesha mchana kweupe.
5 comments:
Km hukwenda police siku hiyo hiyo kabla ya kwenda hospital, achana nao na ushike njia yako.
Mshukuru Muumba wako ungali hai na hujavunjika popote. Wako wanawake wengi siku moja utampata mmoja mwenye hekima atakae ridhika na khali yako ya maisha.
Cha muhimu vuta muda kabla hujaanza uhusiano mwingine ili siku ukiwa tayari, unakuwa mtu mpya ulikwisha msahau Grace kwa kila kitu. Kila la kheri, kuwa jasiri wa kusonga mbele.
Kijana, pole sana. Mambo ya namna hii yametokea kwa wengi, si kwako tu, hasa unapokutana na msichana au mvulana mwenye tamaa, na asiyejua maana ya mahusiano ni nini. Ningalikuwa ni wewe, ningeyoyoma zangu. Hakuna haja ya kuweweseka naye, mwache,usije ukaumia bure. Atajijua mwenyewe huko mbele ya safari.
Wewe mwache utapata mpenzi wako wa kweli usisahau maombi
It is not even worth it fighting for her, mwenye haki ni mungu jiachie uendelee na masiha, na yakimkuta huko wala usimrudie kamwe hata badilike au mtawa, usimkubali kamwe
Mshukuru Mungu.
Post a Comment