ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, November 12, 2013

RAY C ASHEREHEKEA MWAKA MMOJA WA KUACHA UTEJA..!!

SEXY lady wa Bongo Fleva, Rehema Chalamila ‘Ray C’ amesheherekea mwaka mmoja na wenzake tangu alipoacha kutumia madawa ya kulevya ‘unga’.
Ray C akisherehekea na wenzake.

Wikiendi iliyopita Ray C alitupia picha kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram zilizomuonesha akiwa na wenzake katika Hospitali ya Mwananyamala, Dar ambako huwa wanapata dozi ya madawa ya kulevya.
...Akizidi kuburudika baada ya kutimiza mwaka mmoja wa kuacha unga.
Aliandika: “Nawapenda sana hawa wenzangu wote, tuligundua tatizo tukasaidiwa na sasa tumepona na tunamshukuru Mungu...Tanzania bila madawa ya kulevya inawezekana.”

1 comment:

Anonymous said...

Asantge huhitaji kusherehekea unachotakiwa kufanya ni kuendelea kupima afya yako. Unasherehekea ujinga uliokuwa unafanya.Lakini basi pole sana kwa maana ungeendelea mwanangu ungekuta ushaondokaaa. Unaonaje maisha mapya uloiyoanza na wakati ule?