Saturday, November 23, 2013

RIDHIWANI KIKWETE ALAANI SIASA ZA CHUKI ZA CHADEMA ZILIZOFANYA ZITTO NA WENZAKE KUVULIWA MADARAKA

Baadhi ya watu maarufu nchini akiwemo mtoto wa Rais Kikwete, Ridhiwan wamezipokea taarifa za kuvuliwa wadhifa wa unaibu Katibu Mkuu wa CHADEMA kwa Zitto Kabwe kwa mitazamo tofauti.
Zitto alivuliwa uongozi wa Naibu Katibu Mkuu Taifa na Naibu Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kwa tuhuma za kukisaliti chama hicho.
Haya ni maoni ya Ridhiwani Kikwete aliyoiweka katika ukurasa wake wa facebook na twitter kuhusiana na sakata hilo:
Naendelea kujifunza matunda ya Siasa za Chuki na Ukanda zinavyoumiza siasa za Tanzania. Mungu anatuasa kupitia vitabu vitakatifu kuwa ” ili kuepusha balaa dogo kutokea, basi liwe balaa kubwa zaidi ya hilo.”. Imani kuwa aliloandika limetimia… 
Zitto Kabwe pamoja na Dk Kitila Mkumbo watakutana na wahariri na waandishi wa habari kesho Jumapili kuzungumzia hatua hiyo

3 comments:

Anonymous said...

Huyu mtoto hajui alisemalo. Kiongozi yeyote wa CCM hana sifa za kukemea yaliyotokea CDM kwa sababu CCM ndiyo inaongoza kwa siasa hizo. Kwa mwana CCM kufanya hivyo ni unafiki tu!!

Hats off to CDM Central Committee. I am sure you were at critical crossroads. You could either keep the cancerous finger and risk dying of cancer OR chop it off and drastically improve your probability of surviving. You definitely did the right thing in the circumstances. This is now behind you; move on guys!!!

Mdau asiyekuwa mwanasiasa.

Anonymous said...

Ridhiwani, unachotakiwa ni kukaa na siasa ya CCM na wala usiyaingilie haya kwani hiki ni chama kama CCM na kina haki ya kufanya vikao vyake na kutoa maazimio wanayoona yanayumbisha chama, kama CCM wanavyokaa Dodoma usiku wa manane na kuwavua wanachama wasokuw ana hatia!. Acha maneno mengi tunakujua A to Z.!!

Anonymous said...

Huyu mtoto wa raisi mbona ameongea vitu visivyo muhusu wala kuvielewa