Sunday, November 24, 2013

SERIKALI YA NORWAY KWA KUSHIRIKIANA NA SHIRIKA LA HALI YA HEWA DUNIANI (WMO) NA MASHIRIKA MBALIMBALI YA KIMATAIFA YAMEKUBALIANA KUISAIDIA AFRIKA KATIKA KUBORESHA HUDUMA ZA HALI YA HEWA

*KUCHANGIA KATIKA KUKABILIANA NA MABADILIKO YA HALI YA HEWA
*WATAANZIA NA NCHI ZA TANZANIA NA MALAWI.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Dkt. Agnes Kijazi na Mkurugenzi wa utafiti Dkt. Ladislaus Chang’a walishiriki katika hafla fupi ya kusaini makubaliano hayo kati ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani na Serikali ya Norway yaliyofanyika mjini Warsaw Nyumbani kwa Balozi wa Norway nchini Poland tarehe 21 Novemba,2013.
 Kutoka kushoto ni Katibu mkuu wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) Bw.Michel Jarraud, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe; Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Msaidizi wa Katibu mkuu wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) Bi. Elena Manaenkova na kulia kabisa ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) Dkt. Agnes Kijazi katika mkutano wa COP 19 huko Warsaw Poland
Katibu Mkuu wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani alipomtembelea Mheshimiwa Rais katika hoteli ya Bristol tarehe 20 Novemba 2013, alimjulisha kuhusu msaada huo na kwamba Tanzania imechaguliwa kuwa nchi ya awali katika kutekeleza mpango huo kwa imani kwamba TMA itasimamia vyema utekelezaji wake na kupata matokeo mazuri yatakayosaidia kupanuliwa kwa mpango huo katika nchi zingine za Afrika. Kwa upande wake Mheshimiwa Rais alimshukuru Bw. Jarraud kwa misaada ambayo WMO inaisaidia Tanzania na aliahidi kwamba serikali itaendelea kuisaidia Mamlaka ya Hali ya Hewa ili iweze kutekeleza majukumu yake na kushiriki vyema katika program za WMO.

No comments: