Muwakilishi wa Kudumu Balozi Manongi akisisitiza kwamba mabadiliko ya Tabia nchi ( Climate Change) si suala la nadharia kwa sababu yapo matukio mengi yanayoendelea hivi sasa duniani kote ambayo ni dhahiri yanatokana na mabadiliko hayo. akatolea mfano wa Tanzania ambako kumekuwapo na migogoro na hata mapigano ya mara kwa mara kati ya wakulima na wafugaji wakigombea ardhi, maji na malisho. Akasema migogoro kama hiyo ambayo inaathari kubwa kwa jamii za wafugaji na wakulima lakini pia hata kwa serikali kuu. Na kwamba inaweza kuonekana kama ni tatizo la eneo fulani au nchi fulani lakini kama likiangaliwa katika mapana yake dhahiri nyuma yake ni matokeo ya mabadiliko ya tabia nchi. Hata hivyo akasema serikali ya Tanzania inajitahidi sana katika kujaribu kutafuta suluhu kuhusiana na tatizo hilo ambalo anaamini linatokea pia katika nchi nyingine hususani Afrika
Muwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi akizungumza na sehemu ya wanafunzi wanajeshi wanaohudhuria mafunzo ya miezi kumi katika Chuo cha Kijeshi cha Marekani kupitia International Fellows Program, wanafunzi hao akiwamo Luteni Kanal Francis Ronald Mbindi kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) walifika katik Uwakilishi wa Kudumu ikiwa ni sehemu ya zaira ya mafunzo ili kujifunza masuala mbalimbali ya kitaifa na kimataifa ambayo ni vipaumbele vya Tanzania. Kushoto kwa Balozi Manongi, ni Naibu Muwakilishi wa Kudumu, Balozi Ramadhan Mwinyi.
Luten Kanali, Francis Ronald Mbindi kutoka JWTZ akitoa neno la shukrani kwa niaba ya wenzake baada ya mazungumzo yao na Uongozi wa Uwakilishi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa.
4.IMG-4708. Luteni Kanal Francis Mbindi akimkabidhi kwa niaba ya wenzake, Balozi Tuvako Manongi, sehemu ya hotuba maarufu ya Rais Abraham Lincolin aliyoitoa Novemba, 19, 1863 katika maadhimisho ya miaka 150 ya GettysBury ( The turning Point :the 150th Anniversary of the Gettysbury address) hotuba hiyo ya Rais Lincolin inayohesabika kama hotuba muhimu sana kuwahi kutolewa na Rais Lincolin ilikuwa ikielezea kuhusu vita vya wenyewe kwa wenyewe ( CIVIL War). vita hivyo vilivyotokea katika eneo hilo la GettysBury vinaelezewa kama vita vilivyokuwa na umwagaji mkubwa wa damu, ambapo inasadikiwa zaidi ya wanajeshi 50,000 waliathirika ama kwa kupoteza maisha, kuchukuliwa mateka, kujeruhiwa au hawakujulikana waliko
Balozi Manongi akizungumza na mmoja wa wageni
Juu na chini ni Wageni wetu wakipeana na kusaini kitabu cha wageni, hawa wote ni wanajeshi katika ngazi ya maafisa , hawakuhitaji kukaa mezani ili kusaini kitabu
1 comment:
Mwandishi hebu kuweni makini kucheki hata vitu vidogovidogo tu.
Hua mnafanya makosa ya kimaandishi hadi inaudhi.
Huko GettysBury ndio wapi??
Yeyote mwenye uduchu wa historia ya Marekani atajua ni GETTYSBURG
Mkuu si unaishi huko?
Hujasikia hii kitu?
Post a Comment