Sunday, November 24, 2013

ZIARA YA MAFUNZO YA WANAJESHI KUTOKA US ARMY WAR COLLAGE

 Muwakilishi wa Kudumu Balozi  Manongi akisisitiza kwamba  mabadiliko  ya  Tabia nchi ( Climate Change) si suala la nadharia kwa sababu yapo matukio mengi yanayoendelea hivi sasa duniani kote ambayo ni dhahiri yanatokana na  mabadiliko hayo. akatolea mfano wa Tanzania ambako kumekuwapo na  migogoro na hata mapigano ya mara kwa mara  kati ya wakulima na wafugaji wakigombea  ardhi,   maji na malisho. Akasema migogoro kama hiyo ambayo inaathari kubwa kwa jamii za wafugaji na wakulima lakini pia hata kwa serikali kuu.  Na kwamba  inaweza kuonekana kama ni tatizo la eneo fulani au nchi fulani lakini   kama likiangaliwa katika mapana yake   dhahiri  nyuma yake ni matokeo ya   mabadiliko ya tabia nchi.  Hata hivyo akasema serikali ya Tanzania inajitahidi sana katika kujaribu kutafuta suluhu  kuhusiana na tatizo hilo ambalo anaamini linatokea pia katika nchi nyingine hususani  Afrika
 Muwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi akizungumza na sehemu ya wanafunzi wanajeshi wanaohudhuria  mafunzo ya miezi kumi katika  Chuo cha Kijeshi cha Marekani kupitia International Fellows Program, wanafunzi hao akiwamo Luteni Kanal Francis Ronald Mbindi kutoka Jeshi la  Wananchi wa Tanzania  (JWTZ) walifika  katik Uwakilishi wa Kudumu ikiwa ni sehemu ya  zaira ya mafunzo ili kujifunza  masuala mbalimbali ya kitaifa na kimataifa ambayo ni vipaumbele vya Tanzania. Kushoto kwa Balozi Manongi, ni  Naibu Muwakilishi wa Kudumu, Balozi Ramadhan Mwinyi.
 Luten Kanali,  Francis Ronald Mbindi kutoka  JWTZ akitoa neno la shukrani kwa niaba ya  wenzake baada ya mazungumzo yao na  Uongozi wa  Uwakilishi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa.
4.IMG-4708. Luteni Kanal  Francis Mbindi  akimkabidhi  kwa niaba   ya wenzake, Balozi Tuvako Manongi,  sehemu ya  hotuba maarufu ya Rais Abraham Lincolin aliyoitoa  Novemba, 19, 1863 katika maadhimisho ya miaka 150 ya GettysBury  (  The turning   Point :the 150th Anniversary of the Gettysbury address) hotuba hiyo ya   Rais Lincolin inayohesabika kama hotuba muhimu sana  kuwahi kutolewa na  Rais Lincolin  ilikuwa ikielezea kuhusu vita vya wenyewe kwa  wenyewe ( CIVIL War).  vita hivyo vilivyotokea katika eneo hilo la GettysBury  vinaelezewa kama vita vilivyokuwa na umwagaji mkubwa wa damu, ambapo inasadikiwa zaidi  ya wanajeshi 50,000 waliathirika ama kwa kupoteza maisha,  kuchukuliwa mateka,  kujeruhiwa au hawakujulikana waliko
 Balozi Manongi akizungumza na  mmoja wa  wageni
 Juu na chini ni Wageni wetu  wakipeana   na kusaini  kitabu cha wageni, hawa wote ni wanajeshi katika ngazi ya maafisa , hawakuhitaji kukaa mezani ili kusaini kitabu

1 comment:

Anonymous said...

Mwandishi hebu kuweni makini kucheki hata vitu vidogovidogo tu.
Hua mnafanya makosa ya kimaandishi hadi inaudhi.
Huko GettysBury ndio wapi??

Yeyote mwenye uduchu wa historia ya Marekani atajua ni GETTYSBURG
Mkuu si unaishi huko?
Hujasikia hii kitu?