
Ziggy Dee msanii toka Uganda aliyetamba na Eno Mic akiwa studio za Kapestone-Tabora

Ziggy


Pro. BK Mavinanda

Producer EiZeR BiT kwenye mashine

Kushoto: Producer EiZeR BiT, Ziggy Dee na Pro. BK mavinanda.

Producer EiZeR BiT

Wadau wa ukweli kwa pozi

Appson, Ziggy Dee na Stone Wa Kitaa [wa kulia] - wote wasanii

Ziggy Dee na Ma-Producer wake.
Ziggy, ni msanii pekee wa kimataifa ambaye ni mara yake ya kwanza kuingia katika mkoa wa Tabora na kufanya wimbo unaoisifia mkoa huo, katika wimbo wake aliouita LIVINGSTONE CITY amedai kuwa kihistoria katika vitabu vinavyosomwa kwingi Tabora imekuwa ni sehemu maarufu kama moja ya njia na kituo maarufu cha biashara za zamani ikiwemo ya utumwa na Tabora ikiwa ni moja ya Trade routes maarufu, lakini ikumbukwe pia Dr. Livingstone alipita Tabora enzi za harakati za kuutokomeza utumwa na kumkuta mwarabu aliyejihusisha na biashara za utumwa na kumpa habari ya kuachana na utumwa.Licha ya historia ya pekee ya mkoa wa Tabora, msanii huyu amezungumzia kuwa haijalishi kuwa yeye ni wa Uganda lakini sisi sote ni ndugu tunaostahili kujivunia tunu hiyo, amedai kufurahi kufika Tabora kwa mara ya kwanza ikiwa alipafahamu tu kwe history na hatimaye ameandika historia ya kufika eneo husika na kutaka kuacha historia kwa wimbo ambao ataufanyia video yake mapema kabla hajaondoka.
Kazi nzima ya kurekodi wimbo imefanywa katika studio ifahamikayo kama KAPESTONE chini ya Ma-Producer wakali EiZeR BiT na BK (Baraka mavinanda). Ngoma hiyo ina mahadhi ya Raga na inatarajiwa kutambulishwa mapema hivi leo au kesho pindi tu itakapokamilika kwani iko kwenye hatua za mwisho.
1 comment:
Thank you...
Best Regards bro
Post a Comment