ANGALIA LIVE NEWS

Friday, November 15, 2013

WATUHUMIWA WA MENO YA TEMBO ZANZIBAR WAONGEZEKA

Na Mohammed Mhina wa Jeshi la Polisi-Zanzibar
ZANZIBAR NOVEMBA 15, 2013. Jeshi la Polisi Zanzibar limewakamata watuhumiwa wemgine watatu wakiwemo Maafisa wawili wa Mamlaka ya Mapato nchini TRA kituo cha Bandari Zanzibar kwa kuhusika na kashfa ya kupatikana kwa meno ya tembo yenye thamani ya Mabilioni ya shilingi.
Kamishna wa Polisi Zanzibar CP Mussa Ali Mussa, amewataja Maafisa hao wa TRA waliokamatwa kuwa ni Omari Hamad Ali(50) na Mohammed Hija(48) ambao wote wanafanyia kazi katika Bandari ya Zanzibar. Mtuhumiwa mwingine ni kibarua wa Mamlaka ya bandari Zanzibar Haidar Ahmad Abdallah(54).
Kukamatwa kwa watuhumiwa hao kunaifanya idadi ya watuhumiwa waliokamatwa hadi sasa kwa kuhusika na sakata hilo kufikia watano.
Kamishna Mussa amesema Watuhumiwa wengine wawili ambao ni wafanyakazi wa Kampuni ya Uwakala wa Mizigo ya Island Sea Food Limited, Mohammed Suleiman Mussa(45) na Juma Ali Makame(34) wao walikamatwa siku ya tukio la kukamatwa kwa meno hayo ya tembo kwenye Bandari ya Zanzibar.
Tayari watuhumiwa hao wamesafirishwa kwenda Makao Makuu ya Polisi Dar es Salaam kwa ajili ya mahojiano zaidi.Pamoja na mambo mengine, kusafirishwa kwa watuhumiwa hao kwenda Jijini Dar es Salaam, kunatokana na Zanzibar kutokuwa na Sheria maalumu inayohusu wanyamapori. 
Maafisa wa Idara ya Wanyamapori nchini, leo wamekamilisha kazi ya kuhesabu na kulinganisha vipande 1,023 vya meno ya tembo vilivyokamatwa jana kwenye Bandari ya Zanzibar na kubaini idadi ya tembo waliouawa kuwa ni 305.
Meno hao yenye uzito wa kilo 2,915  yenye thamani ya Dolla 4,775,000 sawa na shilingi 7,480,125,000 za Tanzania (Bil.7.4), yalikamatwa juzi yakiwa yamehifadhiwa katika magunia 98 na kuwekwa kwenye konteina moja la futi 40 lenye namba PCIU 857619/0 lillilokuwa tayari kupakiwa kwenye meli ya MV Kota Henning kupelekwa nchini Ufilipino kwa magendo. 
Hadi sasa bado Makachero wa Polisi wa Kimataifa Interpol hapa nchini kwa kushirikiana na Makachero wa Polisi Zanzibar, idara ya wanyamapori makao makuu wanaendelea na upelelezi wa kuwabaini wale wote waliohusika na kashfa hiyo.
Jana Kamishna wa Polisi Zanzibar CP Mussa Ali Mussa, alisema kuwa kazi kubwa iliyobaki ni kuhakikisha kuwa upelelezi wa kina unafanyika ili kuwakamata wale wote wanaohusika na mtandao huo.
Alisema hadi sasa Jeshi la Polisi bado linamsaka tajiri aliyewezesha mipango ya kukusanywa na kusafirisha shehena hiyo kutoka Tanzania Bara hadi Zanzibar ili kusafirishwa nje ya nchi.

4 comments:

Anonymous said...

HUU sio wakati wa kuoneana huruma, bado hamjatuonyesha hao watuhumiwa mmeficha nyuso zao. Na isitoshe si ajabu wanashirikiana na watu wenye majina kwa maana hadi hayo meno kuwa mengi kiasi hicho walipewa mwanya wa kuwaua hao tembo bila kukamatwa!! Wnatakiwa kubanwa ili kuwapata wengineo wenye mali na kutolewa hukumu wazi sio kutuficha.

Anonymous said...

Badilisheni hukum yoyote akikamatwa na meno ya tembo akatw miguu yite na mkono mmoja tuone atauwa sje tembo ns mjichunge saana hiyonndio faida ya wachina miaka yooote wako warabu wahindi na wazungu hakukua msmbo yotee haya bado waanze kuguua na sisi

Anonymous said...

SIASA YA CCM NDO YA KUFICHANA BWANA MLALAHOI HAONI NDANI WACHE WAFICHANE SI NDO NCHI YAO NA CHAMA CHAO CCM OYEEEE UFISADI OYEEE

Anonymous said...

jamani kweli hii ni sawa kati ya waliolamatwa ni anko wangu silalamiki kwanini amekamatwa lakini jambo moja alikuwa amelazwa hospitali amepata mini stroke, alikaa hospitali kwa siku mbili ametolewa nov 13 na kushikwa nov14, cha kusikitisha ni kwamba anatakiwa kurudi hospitali kwa ajili ya follow up na pia hao polisi wamemyang'anya kila kitu mpaka dawa zake. HUU KWELI NI UUNGWANA????? Anko mwenye kati ya hao ni huyo kibarua kweli jamani haki iko wapi,Na wamuweke ndani ila tunachoomba tuu serekali itizame na afya yake au lengo lao ni kumuua kijanja ili kupoteza ushahidi????