Wazazi wa Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, Mzee Kabwe Zuberi na Shida Salum.
Dar es Salaam. Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe, jana alisindikizwa na wazazi wake pamoja na wasanii mbalimbali wa muziki wa kizazi kipya katika mkutano wake wa kwanza na waandishi wa habari aliouitisha baada ya kuvuliwa nyadhifa zake zote ndani ya chama hicho. Tangu alipoanza kupata umaarufu katika medani ya siasa, mbunge huyo hajawahi kuonekana hadharani akiwa na baba yake mzazi, Zuberi Kabwe, bali mama yake Shida Salum ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema.
Mbali ya wazazi hao, wasanii maarufu waliokuwapo ni Peter Msechu, Selemani Msindi (Afande Sele), Mwasiti Almas, Mwanahawa Abdul (Queen Darleen) na Clayton Revocatus (Baba Levo).
Wanamuziki hao ni miongoni mwa wanaounda kundi la Kigoma All Stars ambalo Zitto ametoa mchango mkubwa katika kuliendeleza.
Pia kulikuwapo wakereketwa wa Chadema ambao baadhi yao walimuuliza maswali. Mmoja wao alitaka Zitto aeleze ni kwa nini alivitaka vyama vya siasa vipeleke hesabu kukaguliwa na Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG).
Alihoji kuwa kwa kuwa kiongozi huyo alikuwa ndiye Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), pia Naibu Katibu Mkuu wa (Chadema), alikuwa na nafasi ya kuwaarifu wengine ndani ya chama chake kabla ya kufika hatua ya kutoa tamko kwa umma.
Akijibu swali hilo, Zitto alisema licha ya kuwa kufanya hivyo siyo utawala wa sheria na kutokutenda haki kwa vyama vingine, pia aliwahi kulizungumzia mara kadhaa ndani ya vikao vya chama.
“Nendeni mkawaulize kama mpaka leo mimi ni mmoja wa watu wanaotia saini utoaji wa fedha, nilijitoa baada ya kuona mambo hayaendi vizuri na nikahoji bila majibu,” alisema.
Mwananchi
2 comments:
kumbe wazee wake waislamu na yaye mkiristo siyo tujuzuni please
KUMBE MTOTO WA KIISLAMU ZITTO SO KWA NINI HAFOKI FOKI HUKO BUNGENI KUTETEA MASLAHI YA WAISLAMU NA HASA HASA SIKU YA IJUMAA WATU WAPATA SIKU YA KWENDA KUSALI KWAMA WENZAO SIKU YA JUMAPILI KAZI KUFOKA FOKA OVYOO BILA MPANGO NA DINI YAKE KAIKALIA MAKALIONI
Post a Comment