ANGALIA LIVE NEWS

Monday, December 16, 2013

AIRTEL YAPIGA TAFU TIMU YA TAIFA YA VIJANA CHINI YA MIAKA 17

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Slaa (kushoto) akimuongoza mchezaji wa zamani wa Manchester United Andy Cole kwenda kuwafunda vijana wa timu ya Taifa chini ya miaka 17. Shughuli hiyo ilifanyika jana Dar es Salaam katika viwanja vya Karume mara baada ya mchezaji huyo kuzuru/kutembelea ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania. Wa pili kulia ni Mkurugenzi wa Airtel Tanzania Bwana Sunil Colaso.
Mchezaji wa zamani wa klabu ya Manchester United Andy Cole (kulia) akiwasalimia vijana chini ya miaka 17 kabla ya kukutana na timu ya vijana ya Taifa chini ya miaka 17 katika viwanja vya Karume jijini Dar es Salaam. Wa pili kulia ni Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Slaa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania Bwana Sunil Colaso (kulia) akitoa hotuba fupi muda mfupi kabla ya kukabidhi mipira 100 kwa timu ya Taifa ya vijana chini ya miaka 17 jijini Dar es Salaam jana. Wa pili kulia ni Mchezaji wa zamani wa Manchester United Andy Cole na Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Slaa (wa pili kushoto).
Mchezaji wa zamani wa Manchester United Andy Cole (wa pili kulia) akisisitiza jambo kabla ya kujumuika na vijana wa timu ya Taifa chini ya miaka 17 jana - Dar es Salaam. Wengine ni Mkurugenzi mtendaji wa Airtel Tanzania Bwana Sunil Colaso na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, Jamal Malinzi.
Meya wa Manispaa ya Ilala (wa pili kushoto) akikabidhi mipira iliyotolewa na Kampuni ya Mawasiliano ya Airtel Tanzania kwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania Bwana Jamal Malinzi (kushoto) katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam. Wa pili kulia ni mchezaji wa zamani wa klabu ya Manchester United Andy Cole na Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Sunil Colaso (kulia).
Meya wa Manispaa wa Ilala Jerry Slaa akipiga mpira katika hafla iliyoandaliwa na Airtel jana kukabidhi mipira 100 kwa timu ya Taifa ya vijana chini ya miaka 17. Anayeangalia (kushoto) ni Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania Bwana Jamal Malinzi.

KAMPUNI ya Airtel Tanzania imeahidi kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuendeleza michezo nchini ili kuleta ufanisi katika sekta ya michezo.

Akizungumza kabla ya kukabidhi mipira 100 kwa timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 17 jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Airtel Tanzania Bwana Sunil Colaso alisema uwekezaji katika michezo ni mhimu hasa katika kipindi hiki amabacho Tanzania inajipanga kushiriki katika mashindano ya kikanda na kimataifa.

“Airtel Tanzania tunakabidhi mipira 100 kwa timu ya Taifa ya vijana chini ya miaka 17 kama sehemu ya juhudi zetu kusaidia maendeleo ya michezo.

“Tutaendelea kushirikiana na Serikali pamoja na wadau wengine kuhakikisha nchi inapata mabalozi wa kutuwakilisha vizuri katika mashindano ya kimataifa” alisema

Colaso alisema mwaka 2011 kampuni yake kwa makusudi ilianzisha Airtel Rising Stars ikiwa ni mpango wa kuvumubua na kuendeleza vipaji kwa vijana wadogo kutoka ngazi ya chini ili kuwapeleka ngazi za kimataifa.

Wakati wa hafla hiyo, mkongwe wa klabu ya Manchester United Andy Cole aliwaasa vijana hao chini ya miaka 17 kuongeza bidii ili kutimiza ndoto zao za kucheza kwenye timu kubwa duniani.

“Nimeona vipaji vingi Tanzania. Wachezaji wanaweza kabisa kuchezea klabu kubwa kama wataongeza bidii katika mazoezi yao. Naomba nichukue nafasi kuwakumbusha wachezaji chini ya miaka 17 kuwa na nidhamu si ndani tu ya uwanja bali na nje ya uwanja kwani hiyo ndio nguzo ya mafanikio” Alisema.

Nae Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Slaa aliwashukuru kampuni ya Airtel Tanzania kwa juhudi zake endelevu kusaidia michezo na kutoa wito kwa makapuni mengine kuiga mfano wa Airtel katika kusaidia michezo

“Tunahitaji nguvu za pamoja kati ya sekta binafsi na umma kama kweli tunataka maendeleo katika michezo. Nawashukuru sana Airtel kwa mchango wao katika michezo, niwaombe makampuni mengine waige mfano huu katika kusaidia juhudi za Serikali kuendeleza michezo.

No comments: