ANGALIA LIVE NEWS

Friday, December 6, 2013

KIFO CHA MANDELA-KISWAHILI VERSION

Nelson Mandela afariki dunia: Ban atuma rambirambi

Nelson Mandela, Rais wa kwanza mweusi Afrika Kusini amefariki dunia. Alikuwa na umri wa miaka 95. Kifo cha Mandela kimetangazwa na Rais Jacob Zuma kupitia televisheni ya nchi hiyo.

Kufuatia kifo hicho Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amezungumza na waandishi wa habari mjini New York..

(Sauti ya Ban Ki-Moon)

"Nimesikitishwa sana na Kifo chake. Kwa niaba ya Umoja wa Mataifa natuma risala za rambirambi kwa wananchi wa Afrika Kusini na kwa familia yake pia. Wengi duniani waliguswa kwa kiasi kikubwa na
harakati zake za kugombea utu wa binadamu, usawa na uhuru. Aligusa maisha ya kila mmoja wetu kwa aina yake. Na wakati huo huo hakuna kwa wakati wetu kama yeye ambaye alisongesha maadili na matumaini ya
Umoja wa Mataifa. Alikuwa na msimamo wa kimaadili uliweza kuvunja kuta za ubaguzi wa rangi."

Bwana Ban amesema alibahatika binafsi kukutana na Mzee Mandela mwaka 2009 ambapo alimshukuru kwa kujitoa kwake na kwamba alivutiwa na vile ambavyo hakuwa mbinafsi katika maisha yake. Dokta Salim Ahmed Salim ambaye alikuwa Katibu Mkuu wa uliokuwa Umoja wa nchi huru za Afrika
anamzungumzia Mzee Mandela.

(Sauti ya Dokta Salim)

Hakika Mzee Mandela atakumbukwa hasa kwa hotuba zake alizotoa ikiwemo hii wakati alipohutubia Umoja wa Mataifa.

(Sauti ya Mandela)

Mzee Mandela alizaliwa mwaka 1918.
Kusikiliza bonyeza hapa

No comments: