ANGALIA LIVE NEWS

Friday, December 6, 2013

BONDIA KING CLASS MAWE KUZIDUNDA NA KASHINDE DESEMBA 31 MSASANI KLABU

Na Mwandishi Wetu

BONDIA Ibrahimu Class 'King Class Mawe' ameingia kambini kwa ajili ya mpambano wake utakaofanyika desemba 31 siku ya kufunga mwaka katika ukumbi wa msasani klabu ambapo atatupiana makonde na Mohamed Kashinde katika mpambano wa raundi sita siku hiyo


akizungumza na waandishi wa habari kocha wa kimatafa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' amesema kuwa king class kesha ingia kambini kwa ajili ya mpambano uho wa kufunga mwaka kwani ndio itakuwa mpambano wa mwisho kabisa kwa mwaka uhu


bondia king class mawe yupo fiti na ana juhudi binafsi ya kujituma mazoezini ndio siri ya mafanikio aliyo nayo mpaka sasa na kuweza kuwachachafya mabondia mbalimbali nchini ikumbukwe kuwa class ni bondia chipkizi lakina amesha wachakaza mabondia wakongwe kama Amosi Mwamakula,Simba Watunduru na Said Mundi wa Tanga na Patrick Kavako wa Morogoro ambao wote hawo kawachakaza kwa vipindi tofauti hivyo Kashinde ajiandaee sana

kwa ajili ya kupambana na King Class Mawe

Katika mchezo huo kutakuwa na michezo mingine ambapo bondia Iddy Mnyeke ataoneshana ubabe na Cosmasi Cheka,Antony Mathias akizipiga na Fadhili Majiha katika mchezo mwingine ni kati ya Fransic Miyeyusho wa Tanzania akizichapa na David Chalanga kutoka Kenya

Katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi pamoja na kutambua sheria zake zikiwa na mabondia wakali kama vile
Manny Paquaio, Saul 'canelo' alverez ,Floyd Mayweathar,Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex Trinidad,Miguel Cotto na wengine wengi
pia kuta kuwa na vifaa vya mchezo huo vitakaokuwa vikitolewa na Super D kwa mabondia watakaofanya vizuri siku hiyo na vingine kuuzwa kwa pesa taslimu na kocha huyo kwa ajili ya kuamasisha ngumi

No comments: