Katibu muenezi wa CCM DMV akisherehesha mkutano wa CCM uliofanyika Jumapili Dec 15, 2013 Langley Park, Maryland na kujadili mambo mbalimbali ikiwemo uchaguzi mdogo wa wa Mwenyekiti wa Vijana CCM DMV na Katibu umoja wa wanawake CCM DMV katika mkutano huo walihudhuria Katibu wa CCM New York Bwn. Shaban Mseba akiambatana na Kada mashuhuri wa CCM New York Bwn. Seif Akida.
kuotoka Kushoto ni Aunty Grace, mweyekiti wa CCM DMV Bwn. George Sebo akiwa na katibu wa chama hicho DMV bw. Jacob Kinyemi wakifuatilia mkutano
Wanachama waliofika kwenye mkutano huo wakisimama kwa dkk 1 kumkumbuka Mzee Nelson Mandela.
Mwenyekiti George Sebo akiongea machache.
Katibu wa CCM New York Bwn. Shaban Mseba akileta salamu kutoka CCM New York.
Ismail Mwilima mwenyekiti wa vijana CCM DMV akijinadi kabla hajachaguliwa kwenye mkutano huo.
Katibu muenezi Salma Moshi (kulia) akisaidia kumnadi Mariam Kachingwe ambaye alishinda na kuwa katibu wa umoja wa wanawake CCM DMV.
Juu na chini wanaCCM DMV wakifuatilia mkutano.
Picha ya pamoja
kwa picha zaidi bofya soma zaidi
14 comments:
Watanzania DMV tupo zaidi ya 2000. Lakini hiyo picha ya pamoja ndiyo idadi ya wana-CCM DMV. Na hapo kunawageni toka states zingine. Kwa nini idadi ya wana-CCM DMV haiongozeki?????????????????????
Hapa ndugu zangu lazima kieleweke. Ndugu yetu Mtanzania aliomba asaidiwe kusafirisha mwili wa baba yake,na tuliombwa wote tukutane hili tuweze kumsaidia. Cha kushangaza CCM.....wamegawa watu kwakuandaa mkutano wao sambamba na maombi ya mfiwa...kulikuwa na haraka gani ya huu mkutano wa CCM hapa DMV? Ccm au vyama vya siasa vinamuongoza nani hapa USA..nakwingineko?...kwakweli imeniuma saana nikiwa kama MTANZANIA......
Swali hilo la "Kwa nini idadi haiongezeki" ni la kinafiki na halina tija. wewe uliyeona kuwa idadi haiongezeki unaweza kuwa na jawabu lake badala ya kuuliza katika mfumo wa kinafiki. Ungetoa takwimu kuwa mkutano Fulani walikuwa wanachama kadhaa, na mwingine walikuwa kadhaa na vipi huu wawe idadi kama ya ile mingine? Hapo ungeuwa unaongea itakwimu na ungeeleweka. Hii si tabia nzuri!
Swali zuri sana mdau. WE DO NOT NEED VYAMA HUKU UGHAIBUNI, HATA MWANZILISHI WA CHAMA HICHI MWALIMU NYERERE ALIYEKUWA ANAKUJA MAREKANI MARA CHUNGU NZIMA HAKUWAHI KUVAA KIJANI NA KUPIGA PICHA NA WANACCM NA WALIKUWEPO. But utamwona akifika bongo ndo utamtambua kuwa ni mwenyekiti wa CCM. Hivi vyama sijaona wanachokifanya hata kupeleka madawati,vitabu, madawa hatujasikia. HAYA NDO YANAYOWAKERA WANANCHI BONGO. Sisi tupo huku tukutane kama Watanzania katika profession zetu tuone tutasaidiaje nchi yetu. Wenzetu wawest nasikia kuna vikundi vya manesi na madaktari vinakwenda Africa kila mwaka kutoa MOBILE MEDICAL SERVICE kwa wananchi kujua kuwa waafrica hawafanyi medical check-up. So wanakwenda kuhamasisha vijijini wanapima kina mama, kina baba na watoto kila kitu bure. It needs few positive minds to make changes in our country kama tukiungana kama watanzania. Mpasuko wa vyama huku ughaibuni unatudhaifisha sisi kama Waafrica kutwa ni kuongelea CHADEMA NA CCM. WHAT ARE WE DOING TO OUR COUNTRY? Watoto wanasoma katika mazingira magumu lets all contribut $10 TUNUNUE TAA ZA SOLAR TUKADONATE VIJIJINI ILI WALE WATOTO WWAWEZE KUSOMA USIKU na kuwa na upeo. Au tukusanye pesa tukainstall solar systems mahospitalini maana hizi ndo issue muhimu bila kujali wewe ni ITIKADI GANI. Tangu vyama vimeanza ushabiki hapa mjini ni vikao tuu tunaviona lakini hatuoni wanachofanya! TUBADILIKE WAJAMENI.
Tafuteni kazi mufanye Kama mnataka siasa rudini kwenu Tanzania
Wewe mnafki wa madawati ccm tumenza nia nikusaidia sasa wewe unaharaka lete mchango wako ccm ipo taka usitake
Mdau uliyeuliza swali nakupongeza sasa. Lazima CCM-DMV wakubali kuwa kuna tatizo. Kama hawakubali na kuliona hilo tatizo, basi na hilo nalo ni tatizo.
Kamanda Benja yuko wapi? Au na yeye amechakachiliwa?
Good on you all, haya ma-vyama ughaibuni hayana lolote, total waste of time and resouces! Labda tutakuwa na Senator from CCM in the USA Senate, good luck!
Haters Kama kawaida yenu tumewazoea, Nani aliwaambia kelele za chura zamzuia ng'ombe kunywa maji? Inaonekana ni jinsi gani msivyokua na kazi za kufanya , kutwa kucha kutoa negative comments Kwenye Vijimbambo, Seriously, hamna kazi za kufanya? Mnapata wapi huo muda wa kuchafua????? Badilikeni bana Watu wazima nyie tena mko abroad mna exposure mbona mna behave Kama mmetereka Leo Kwenye reli ya Kati. Download a time management Apps called "MIND YOUR OWN BUSINESS"
robo you waliohudhuria ni watoto
Hivi Wabongo aka Watanzania tutaanza kupendana lini jamani?? Majungu,fitina, unafiki, makundi, na ubaguzi ndo maisha yetu ya DMV. Acheni kujigawa kwa majina jamani (USHAMBA HUO), mnakwenda misibani ka majina? shame on you!Kweli Mungu hapendi...TUBADILIKE....
Yawezekana. Hivi vyama UKISEMA UKWELI TU, unachakachuliwa. MAKUBWA.
MAJANGA!! Huyo aliyeleta hii idea ya vyama kweli anastahili adhabu! NATAKA KUULIZA VYAMA VINATUSAIDIA NINI??? KURA HATUPIGI HUKU UGHAIBUNI NA WANGAPI WANA MAKARATASI YA KUWAWEZESHA KURUDI NYUMBANI KUPIGA KURA AU KUGOMBEA CHEO CHOCHOTE? HEMBU TUAMBIANE UKWELI. DUUH wana CCM wamekuwa wakali na majibu yao badala ya kutoa maelezo. Just curious tunaomba data mna wanachama active wangapi? Wangapi walihudhuria kikao. Mdau anayeuliza swali kuwa hamuongezeki anataka kuwasaidia ili mfikirie jinsi gani mtahamasisha watu wawe na mtazamo kama wenu ili mjenge chama imara. So toa majibu with facts ili tuone kama kweli una hoja. Tupe takwimu hatuzijui ndo maana watu wanasema hawa waliopo kwenye picha ndo waliohudhuria.
Post a Comment