Edward Waigama anasikitika kutangaza kifo cha mama yake mzazi kulichotokea usiku wa kuamkia leo Jumatano Dec 11, 2013 Nairobi Kenya alipokuwa amelazwa baada ya kupelekwa huko kwa matibabu.
Kupeana pole ndio mila na desturi yetu. Kwa hiyo upatapo nafasi mpitie mpe mkono wa pole. Msiba upo
704 Clopper Rd Apt 33, Gaithersburg, MD 20878
Au mpigie namba yake ya simu ni 240 899 6900 au 240 899 2333
Edward Waigama anatarajia kusafiri kwenda Tanzania kuungana na wanafamilia wengine Jumamosi Dec 14, 2013.
Kwa hiyo ndugu zangu tujumuike na ndugu yetu Edward katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mpendwa mama yake.
Bwana ametoa, Bwana ametwaa na jina lake lihiimidiwe.
No comments:
Post a Comment