ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, December 26, 2013

MSICHANA MMOJA APOTEZA VIDOLE NA WATU 60 WAJERUHIWA NA SAMAKI AINA YA PIRANHA KWENYE MTO PARAMA, ARGENTINA

Licha ya kibao cha kukataza watu kuongelea kwenye mto  huu wa Parama watu 60 wajeruhiwa na samaki aina ya Piranha na msichana mmoja kupoteza vidole vya miguu. Watu hao walikuwa wanasherekea sikukuu ya Krismas kwa kuogelea ndani ya mto huu. Samaki huyo aina Piranha ni mwepesi wakushambulia ukiwa unaogelea na sehemu rahisi kwake kujeruhi ni vidoleni.
Huu ndiyo mji wa Rosario huko Argentina ambako watu walijeruhiwa na Samaki aina Piranha wakila bata la Krismas. Tukio kama hilo limeshawahi kutokea mwaka 2008 na watu 40 walijeruhiwa na samaki huyo anayesemakana kuwa ana meno makali sana.
Huyo ndiyo samaki alieleta maafa huko Argentina wakati watu wakila bata la Krismas katika mto Parama katika mji wa Rosario.

No comments: